MADHARA YA UCHIMBAJI DHAHABU KWA WATOTO WADOGO
mgodi wa geita chanzo cha picha Wavuti - Weebly |
Dhahabu
ni aina ya madini yanayo patikana ardhini na madini haya huwa na thamani kubwa
ukiacha Almasi pamoja na madini ya tanzanite. Katika nchi ya Tanzania madini haya
hupatikana kwa wingi katika mikoa ya kanda ya ziwa kama vile Mwanza,
Geita,Mara,Shinyanga na maeneo mengine kama vile Singida, Mbeya, Katavi na
sehemu nyinginezo za Tanzania ambapo madini aina ya dhahabu yana patikana.
- Katika mkoa wa geita wenye jumla ya wilaya nne [4] ambazo ni wilaya ya Geita mjini, wilaya ya Mbogwe, wilaya ya Nyang’wale pamoja na wilaya ya Bukombe. Wakazi wengi wa mkoa wa Geita hujihusisha na shughuli za kilimo .kwa asilimia 70% ya wakazi wa mkoa wa geita hutegemea kilimo huku asilimia 30% hujihusisha na shughuli za uchimbaji dhahabu.Pamoja na shughuli nyingine.
- Katika hali isiyo ya kawaida watoto wengi wenye umri chini ya miaka kumi na nane hujihusisha na shughuli za uchimbaji dhahabu katika maeneo yenye shughuli hizo za madini watoto hao mara nyingi hufanya shughuli za kuosha mchanga wenye dhahabu, kuponda mawe yenye dhahabu,kusimamia makarasha[kifaa kitumikacho kusanga mawe yenye dhahabu], wengine huchimba mashimo ili kuweza kupata dhahabu, wengine huuza maji,chakula,sigara, karanga katika machimbo ya dhahabu.
- Watoto huathirika kisaikolojia;watoto huweza kuathirika kisaikolojia kwa kuwa hufanya kazi maeneo ambayo ni hatarishi ukilinganisha na umri wao kwani huweza kuingia katika mashimo marefu[maduara] pia vilipuzi kama Baruti hutumika. Hii hupelekea mtoto kuweza kupata madhara ki akili na kimwili hali hii hupelekea jamii na taifa kwa ujumla kuwa na watu ambao hawana utimamu wa akili na mwili.
- Watoto hukosa haki zao za msingi; shughuli za machimbo husababisha watoto kupoteza haki zao za msingi kama vile kupata elimu iliyo bora, kupata malezi ambayo ni bora. vile vile hii husababisha baadhi ya watoto kutumikwishwa kazi ngumu kama vile kuponda mawe, kuosha mchanga wa dhahabu, kuanika mawe pamoja na kusimamia mashine za kusanga mawe na mwisho wa siku hupewa ujira kidogo kama malipo ya kazi wanazo fanya katika maeneo ya uchimbaji dhahabu.
- Hupelekea vifo au uvilema; mara kadhaa kumekuwepo na matukio ya vifo pamoja na watu kupata vilema vya maisha watoto wengi chini ya umri wa miaka kumi na nane hukubwa na umauti aghali wa dogo hii hutokana na mazingira hatarishi wanayo fanyia kazi mfano baadhi ya duara huwa na nyufa ambazo huweza kudidimia zenyewe, baadhi ya duara huwa na gesi kali ambayo hu Ua kwa haraka hivyo basi vifo na ulemavu huweza kuwa kumba watoto wanao jihusisha na shughuli za uchimbaji madini chini ya umri wao.
- Watoto hupata magonjwa; katika maeneo ya uchimbaji dhahabu watoto huweza kupata magonjwa kama vile ukimwi, kipindupindu, na magonjwa ya zinaa kama vile kaswende na kisonono. katika upande wa magonjwa watoto wa kiume na wa kike hujikuta ni waathirika wakubwa. Mfano watoto wakike hulazika kufanya biashara ya ngono ili waweze kupata pesa na kukidhi mahitaji yao pia vijana wa kiume nao huingia katika mtindo huo wa maisha kwa kuiga na mwisho wa siku hujikuta wakipata ukimwi na kuugua magonjwa ya zinaa nahii hupelekea taifa kuingia gharama za ku wahudumia na kushindwa kupiga hatua kama taifa.
watoto wakiwa katika shughuri zao za kila siku mgodini, picha mtandaoni |
Watoto kama Taifa la kesho hawana budi kusaidiwa na kusimamiwa katika mambo yote ambayo yanaweza kuhatarisha maisha yao.Hivyo wazazi na jamii kwa ujumla ya paswa kuungana na kukomesha suala la watoto kujishughulisha na shughuli za uchimbaji dhahabu pamoja na shughuli ambazo zina kiuka haki za msingi za watoto.
MUANDISHI
BUGANGE .M. MTABAZI
2 comments:
Good for lesson
Hakika
Post a Comment