MWALIMU KWANINI UNICHAPE TU?
Charles N Matagi
BARUA KWA MHARIRI
Mpendwa
mhariri,
Mimi
ni Yule mwanafunzi mtukutu na jeuri ambae siendi shule na darasani ni sehemu ya
kifungo kwangu kwani kila ninapojaribu kutafakari masaa manne ya asubuhi nikiwa
darasani kiukweli nachanganyikiwa na mara zote nakiri akili yangu inamuona
mwalimu wa zamu akija akiwa amependeza kwa shati na tai huku akiwa amekamilisha
uhusika wake na kiboko kirefu na kinene kuliko mwili wangu ama kwa hakika napata
tabu.
- Napenda shule, naipenda kweli! ila nnapoikaribia shule kutoka huko mbali niishipo,shule inakuwa mwiba mkali kwangu, kwani mara nyingi nilikuwa nafika saa moja na nusu huku kengele ya namba inakuwa imesha pigwa saa kumi na mbili na nusu hapo ninakua nimeshajihakikishia kipigo safi kutoka kwa mwalimu wa zamu kwani ntakua sina namba ya asubuhi.
- Nakaa mbali hakika nakaa mbali kwanini nisichapwe na mwalimu wa hisabati kwamba nimesinzia darasani katika kipindi chake cha kwanza, kama naamka saa kumi na moja naparangana na mambo mbalimbali kufika shuleni na nikifika shuleni naparangana tena na usafi wa mazingira na taratibu za shuleni ni vipi nitaacha kusinzia nikipata wasaa wa kutulia darasani, hakika mwalimu nipige univunje mimi nitasinzia.
- Ni mimi...yani ni mimi yule ambae ulinitoa darasani katika kipindi chako eti kuwa nililala katikati ya kipindi na nilishindwa kujibu maswali uliyo niuliza baada ya kuniamsha ni vipi nitapata vema katika mtihani wa somo lako? Mwalimu usiishie ofisini kwa walimu wenzio nipeleke kwenye jukwaa kubwa na mnipige wote ila kutoboa kwenye somo lako naamini kwangu ni ngumu.
- Hahahaha shikamoo mwalimu...haukuniona darasani siku kadhaa lakini wala hukuniuliza ulinichapa na kunitangaza kwa walimu wenzio kuwa mimi ni mtoro sana, sasa nimwambie nani shida zangu wakati anaenifanyia hivi ni baba yangu wa kambo? Haya mwalimu nichape labda ndio njia ya kuniweka karibu na wewe chapa mlezi wangu chapa uuwe.
- Ni vipi ntaacha kutamani kuwa kama Zuhura ambae amemkubari bodaboda na sasa kila siku anawaishwa shuleni na kukwepa kichapo kikali kutoka kwako mwalimu, kwakichapo chako unachonipatia kweli bodaboda atanipata.
Ni
mawazo yangu kwamba ili unisaidia mimi mwanafunzi wako mtukutu na mkaidi sana
ambae nashindwa kutulia katika kila hali ambayo wewe mwalimu wangu unataka niwe
basi ungeangalia njia nyingine tofauti na kiboko ambacho umekua ukikitumia kwa
muda mrefu sasa bila mafanikio ya kunisaidia zaidi zaidi kimenifanya nimekua na
hofu na muda wote nimekuwa wa kukuogopa sana kuwa karibu na wewe mwalimu wangu.
Kama utaweka kiboko chini au kupunguza matumizi ya kiboko na kufanya maongezi
pamoja na ufatiliaji vikawa ndo njia yako yakutatua shida ambazo mimi mtukutu
nazifanya basi hakika bodaboda hatonipata, baba wa kambo atonitesa kwa namna
yoyote ile kwani nitakwambia na utanisaidia na nitapata kuwa mwanafunzi mwema
kwako na katika masomo kwani kama ntasinzia ukanipa adhabu ya kusimama katika
kipindi badala ya kunitoa nje basi nitaweza kupata maksi katika somo lako
mwalimu. Naomba ufikirie tena jinsi ya kunisaidia mwalimu.
No comments:
Post a Comment