KATA TAMAA UFANIKIWE……………………
Unajua katika maisha
siku zote kuna njia nyingi za kupita ili ufanikiwe na kikubwa ni kujituma tu
katika majukumu unayoyafanya lakini kuna watu wenye fikra potofu wanafikiri
kwamba njia pekee ya kufanikiwa ni kukata
tamaa kumbe haiko hivyo kabisa kwani
usipokata tamaa na ukaamua kujituma ni kipi kinachopungua kwako kutafuta kwaajili
ya kesho kupo palepale hivyo sizani kama
kukata tamaa ni njia ambayo inaweza ikakutoa katika hali uliyokuwa nayo na
kukupeleka katika hali nzuri pia tamani sana wewe utegemewe kuliko wewe
kutegemea .Pia jambo lingine ambalo vijana wengi hatulifahamu ni kwamba
kutegemewa katika maisha na familia kwa ujumla ni jambo lenye Baraka hata kwa Mwenyezi Mungu kama
unataka kuamini hilo siku pata hela halafu
humtumie mama yako usikie Baraka utakazo zipata kutoka kwa mama hakika
mama anakuwa anafurahi sana anapomuona mwanae anapambana katika maisha kila
siku atazidi kukuombea ili ufikie hatua Fulani .Tena jambo la kijasiri zaidi
mama yuko tayari afanye jambo lolote ilimradi wewe kijana wake ufanikiwe
ijapokuwa anaweza asitake chochote kutoka kwako baada ya wewe kufanikiwa kwani yeye
furaha yake ni kuona wewe tu unafanikiwa sasa wewe unapokata tamaa nini
ufanyiwe?. Je! Tangia ukate tamaa umefanikiwa marangapi katika kukata kwako
tamaa .Siku zote katika maisha jifunze kuwa jasiri katika kila vita
unayopambana kwani ushindi ni kwa wale wanaojituma na kuonesha jitiada katika
safari yao ya kimaisha .Kukata tamaa sio njia ya wewe kufanikiwa na pia jifunze
kwamba hali ngumu yoyote unayopitia sio ya kudumu ni darasa tu unapita ili ujifunze haina maana
kwamba wewe utabaki katika hali hiyo kamwe na njia pekee ya wewe kujitoa katika
hali hiyo ni kuto kukata tamaa na kuwa mvumilivu katika kila kipimo unachopitia
kikubwa ni kuweza kumtegemea Mungu tu kwa kila jambo na siku hizi kuna msemo
usemao kila hatua na dua…………………………………..KUKATA TAMAA SIO NJIA YA KUFANIKIWA
KATIKA MAISHA HATA SIKU MOJA ,KWANI UKIKATA TAMAA HAUTOPATA KITU CHOCHOTE ZAIDI
YA MATESO YA KUDUMU YA KIAKILI..
BY
FADHILI TAJI @ beyond thinker.
No comments:
Post a Comment