Fahamu kuhusu Kiboko mnyama mla nyasi ambae ni atari zaidi mbugani.
Na Charles N Matagi
KIBOKO
Jinasi : kenyapotamus
Familia : hippopotamidae
Kiboko
ni mamalia mkubwa wa familia ya Hippopotamidae, Kiboko uishi kwenye maji pia na
nnchi kavu, ni mnyama wa tatu kwa ukubwa kwa wanyama wapatikanao ardhini
akitanguliwa na Tembo na Kifaru, kiboko akiwa na uzito wa tani 1.5 – 3.5, tembo
akiwa na uzito wa tani 2 - 6 na faru mwenye tani 2 – 4. Kiboko akiwa ni
miongoni mwa wanyama wenye sura ya kipekee ambayo macho,masikio, na pua vyote
vimejipanga juu ya uso wa mdomo wake na anauwezo wa kufungua mdomo wake mpaka
mwisho, sio tu maji Kiboko anaishi kwenye maji baridi ya mto au ziwa, Kiboko
akiwa na urefu wa mita 3.3 mpaka 5.2 mkia ukiwa una sentimita 56, ili ashibe
Kiboko inamladhimu ale nyasi kilo 65 kwa siku na Kiboko anaweza kuishi miaka 45
mpaka 50 kama ato windwa au kuuwawa.
- Kulingana na manyoya yake madogo mno inamladhimu Kiboko kukaa kwenye maji kulikimbia jua na ilikujikinga na jua mchana uwaga anatoa maji mekundu ambayo tunayaita jasho jekundu ambalo umsaidia pia kujizuia na mionzi ya jua kumfikia na Kiboko anatoka kutembea usiku tu kitu kinachomfanya kuwa ni mnyama mla nyasi atari zaidi kukutana nae kipindi cha usiku kwani ndio mda wake wa kujidai, licha ya kuwa simba na mamba ni wanyama wanaofanya majaribio ya hapa na pale kuwinda viboko watoto ila inakuwa ni atari kubwa mama kiboko akigundua mamba amemzuru au amekula mtoto wake kwani kutokana na utata wake kiboko uwashambulia mamba na kuwatoa mbali na ziwa mpaka hali itakapotulia ndipo mamba wanarudi kwa maji.
- Katika masuala ya kutafuta chakula Kiboko ni myama mbinafsi kwani kipindi chakwenda kutafuta malisho kila kiboko huwa anaenda sehemu yake kujitafutia chakula chake mwenyewe.Kiboko jike uacha kukua mala tu anapofikisha umli wa miaka 25, Kiboko maisha yake ya mchana Kiboko utumia muda wote akiwa kwenye maji na pindi jua linapozama utoka na kwenda kutafuta hicho chakula, Kiboko sio kama wanyama wengine wa ardhini yeye kuanzia kujamiiana na kuzaa mambo yote hayo uyafanyia kwenye maji pia wakati maziwa ya mamalia wengine akiwemo binadamu yakiwa ni meupe Kiboko kwake ni tofauti maziwa ya kiboko huwa yana rangi ya pinki maziwa ya kiboko huwa yana rangi ya pinki picha na Insect Safaris Adventures
- Kutafuta chakula Kiboko huwa anaenda kilomita 8 na ni miongoni mwa wanyama mwenye atari kubwa kukutana nae kwani ni mnyama anae wezakuvizia, mkolofi na ni mtata, pia mbishi na kushambulia bila woga pale anapokuwa amemuona adui basi umfuata kupambana nae kitu ambacho kina mfanya Kiboko kuwa mnyama aliefanikiwa kuuwa binadamu wengi zaidi. Hukiachana na miguu yake mifupi inayoonekana kuelemewa na ukubwa wa mwili Kiboko anakimbia kilomita 29 kwa saa kitu kinacho fanya inakua ngumu kwa binadamu kumkimbia kiboko
- Jambo lingine la kushangaza kwa mnyama huyu Kiboko ajui kuogelea ila anauwezo mkubwa wa kutunza mpumzi akiwa chini ya maji na mala kwa mala uja juu kutafutapumzi mala tu inapomuishia pia Kiboko analala akiwa kwenye maji huku akiendelea kupanda na kushuka chini kutafuta pumzi, kiboko anandevu ngumu kama waya ambazo pia uzitumia katika kushambuliana na adui ake akiwa anapambana,
Kumbuka : Kiboko
ni mnyama atari sana kwa maisha ya binadamu na ni mnyama anae uwa vibaya zaidi
kwani Kiboko akikukamata anakuingiza mdomoni nakukubana kiuno na kukutenganisha
tu kiulaisi ivyo usiangaike kupambana nae. Na moto ni kitu pekee anachokiogopa.
(chanzo cha picha mtandaoni)
No comments:
Post a Comment