Breaking News
recent

PENDO LANGU SEHEMU YA KWANZA


By Lazaro nyerere
Image result for black beautyClintoni ndio jina langu nililopewa na wazazi wangu na kwetu tulizaliwa watatu mimi, kaka yangu alieitwa James na mdogo wangu wa kike Jack, Nikiwa na umri wa miaka 21 kaka yangu alifariki. Siwezi elezea sana uchungu niliyoupata kwani sitamani kukumbuka hata kidogo maumivi yale, ivyo tulibaki wawili Mimi na mdogo wangu mpendwa Jack. Baada ya wiki mbili kupita tangu kaka afariki mdogo wangu jack alisafilishwa kwenda singida kusoma na nikabaki na wazazi nyumbani, niliendelea na masomo yangu Kama kawaida, nlikua na hitimu kidato cha sita.
Mbali na masomo na mapambano mengine ya kimaisha lakini Clintoni mimi sikua peke angu nlikua na tunda langu lenye kuvutia sana au ninaweza sema mpenzi wangu wa maisha, ambae tulipendana sana mi na yeye, pia tulijaliana sana na mrembo huyo kwa jina aliitwa Mary, binti alikuwa ni mzuri Sana mrembo mwenye urefu mithili ya twiga mtoto, hakika mtoto mery aliukamata moyo wangu vilivyo, sauti yake nzuri na tamu yenye kuleta hisia na ilio tanadari upendo kwa kuongea hata kucheka kiukweli nilimpenda Sana mery wangu….
Mapenzi yetu yalikuwa yenye furaha Sana, ilipata kupita miezi sita nikiwa na mery huku tabasamu na upendo vikitawala kipindi chote, siku moja tukiwa tunatoka katika moja ya matembezi yetu mimi na mery na huku tukiendelea piga stori za hapa na pale Kama wapenzi tulio shibana.  ikiwa ni mida ya jion Sana huku mery hofu na woga vikianza kumtawala akiwaza itakuaje kama ata chelewa nyumbani na kumkuta baba yake,kama tamaduni nilimtoa hofu kwa na kumuhakikishia nilimpeleka mpaka mlangoni kwao tukaagana na mimi kurudi nyumbani kwa furaha kama yote, kama unavyojua mambo ya njiani tena wakati narudi nyumbani  nlikutana na majaribu.
Mara mwanamke mmoja alikuja kwakasi katika uelekeo wangu kiasi kwamba sikujua ametokea wapi na sikuelewa, akaja nakuanza kujibaraguza kwangu huku akisonga karibu yangu zaidi nakuanza kusema.
“Hellow Mambo vipi,”
 Mimi nikamjibu, poa tu (huku nikitafakari huyu binti katokea  wapi mida hii na ni wawapi?)
Akazidi kunisogelea na kuendelea kusema” kwa muda mrefu sasa ninakuona hapa mtaani uko vizuri Sana unanivutia, kwani wewe ni kijana mtanashati sana na mpole, nimejikuta tu nikikupenda Sana bila kipingamizi. Naomba siku ukipata nafasi uje kwangu hii ni business card yangu utanitafuta muda wowote tafadhari  sana usiache kunitafuta, na  nakutakia siku njema handsome.?
Kweli aliongea mfululizo atasikupata nafasi ya mimi kutupa neon lolote Lile nilimshangaa Sana yule mwanamke kwani bado nlijiona nikijana mdogo sana kwakena nikajiuliza kimoyomoyo “anataka Nini kwangu” nilitembea huku najiuliza maswali mengi sana Kwani kwa muonekano tu wa haraka haraka yule hakua binti alikuwa ni mwanamke wakunizidi Sana na anafaa kuitwa mama lakini kwa dunia ya Sasa wanasema mapenzi hayana mwenyewe Kila mtu anapenda hata Bibi huchukua vijana na aitokua ajabu Sana. Na wanachagiza kwa kamsemokao kakihenga eti “ngombe azeeki maini”
Sikutia akilini sana kuusu hilo lililotokea kwa sababu Nilikua teali nina mpenzi na ananipenda sana, nilifika nyumbani na kunyoosha moja kwa moja chumbani kwangu nikaitupa ile business card kitandani na kuingia bafuni kuoga huku saa ya ukutani ikisoma ni saa mbili kasoro, Mara nkaskia mlango wangu unagongwa kwa nguvu zote sikuelewa ni Nini kilikua kinaendelea hivyo ika nibidi nisimamishe zoezi langu la kuoga Kwanza nikasikilize ni nani kwani ile sauti iliendelea ya kugonga mlango bila kuacha. Wakati natoka mkuku mkuku toka bafuni nkakuta simu yangu ikiita kuangalia alikua ni mery anapiga nikapokea simu na kumwambia,
 “Hellow, mpenzi ntakutafuta mda sio mrefu kuna shida kidogo hapa nyumbani”
Kwa sauti ya chini mery akajibu “Sawa dear lakini usichelewe, poa baadae” (tuliiagana ivyo na nkachomoka kitandani kuelekea mlangoni)
Huku macho yangu yalikuwa mlangoni ile na sauti ikiendelea kugonga mfululizo nkaanza kijifikilia Nina taulo tu nimejifunga linaweza tokea zari lolote maana sio kwa aina ile ya ugongaji, nikiwa katikati ya mawazo hayo nikajikuta nmeufikia mlango na nilifungua mlango kwa tahadhali Sana na nilipo fungua mlango sikukuta kitu chochote niliona nyayo tu Kama za binadam ivyi ila sikua na uhakika sikupoteza mda nilirudi ndani huku roho  yangu ikiwa mkononi,
Daah! Nlirudi nakuendelea kuoga kwa mala nyingine tena, nlimaliza na kutoka bafuni na kiukweli pale nyumbani kulikuwa wapangaji wa kike kadhaa na kiume nikiwemo na Mimi hivyo sikuweza kuelewa ni nani atakua alikua akinigongea mlango kwa mtindo hule hivyo nikapotezea,
Nikachukua simu yangu ya mkononi na nikamtwangia mpenzi wangu Mary tuendelee kuchat kwa maongezi yaani kuongea nae, kabla simu kuita mara ghafla mtu akaingia chumbani kwangu pasina ata kupiga hodi kumwangalia vizuri alikuwa ni Ester mpangaji sijakaa sawa kumuuliza anataka Nini kwangu usiku huo. Mary akawa amepokea simu, ikaniladhimu nimwambie tena nitakutafuta kesho na sio tena usiku huo kwamaana nlikua nishakasirika sana hususani kwa zile kelele za mwanzo na hili la mtu kuingia chumbani kwangu bila kugonga mlango.
Nikaamuliza enheee Ester unataka Nini chumbani kwangu saiz usiku sinakuliza (nlikua mkali kwa kile kitendo kwa sababu nlikua na taulo tu je angenikuta nko mtupu)
Ester hakunijibu Kwanza alikuwa amevaa kangha tu nahisi na ndani hakuwa na kitu, hakunijibu alikuwa akiniangalia kwa jicho flani ivyi ambalo kama unamoyo mwepesi na unahisia za minato unaweza  kutaka kufanya kitu kwake.
“Clinton nimeshindwa kuvumilia nakupenda mwenzako unatesa moyo wangu haipiti siku sijakuwaza na kukufikilia kweli nihurumie mwenzio Clinton jamani nihurumie” Esta aliyasema maneno hayo huku akijaribu kujishika shika baadhi ya sehemu zake muhimu
Bila kuficha ukweli ni kuwa nilimshangaa Sana kwa iyo kauli ya Ester kwa jinsi nlivyokua na mheshimu Kama mpangaji wetu nilimvuta na kumtoa njeee hima hima na hapo sasa saa ilikua inasoma ni mida ya saa tatu. Na muda huo ni Ester ndiye alikua akisumbua akili yangu sana na sikujali nilimtoa nje kwa nguvu nakufunga mlango huku baadhi ya maneno machafu yakinitoka kwa hasira.
Kwa kweli usiku ule haukua mzuri Sana kwangu nilishindwa kisa mlang kuongea na Mary baada ya mlango kugongwa gongwa na Ester akanivurugia  kwa mala ya pili tena nkashindwa kuongea na wangu wa huba, nakili  nililala lakini sikua na amani kabisa.
Asubuhi palipo pambazuka niliamka nakujimwahia maji tena, nikamaliza na kuchukua nguo zangu kabatini nivae ili niende katika mishe zangu, wakati natoka kwangu kuelekea dukani nnakofanya biashara zangu nlikutana na Ester nje akiniangalia Sana na mi nikimwangalia huku nikitikisa kichwa tu kwa kumsikitikia.
Nilipita nyumbani kwa kina Mary nikamuona akiwa amekaa kwenye kibaraza nikaamua kufanya vile vimichezo vya huba hivyo sikumshitua wala kumuita nilienda kwa nyuma na nilimziba macho tu kiaina. Kumbe bwana Mary hakua vizuri siku hiyo hivyo nikamuuliza mpenzi vip mbona unanikatia ivyo wangu, Mary alikuwa kakasirika sana kwa kitendo nilichomfanyia Jana usiku.
Tukiwa tunajibizana pale Ester alipita na kutuangalia hali ya kuwa Mary hajui lolote linalo endelea hivyo aliendelea kuongea tu sikutaka kumkwaza nikamwambia mpenzi samahani jana nilikua na shida kidogo afu sikuweza kuongea na simu kwa wakati ule, Ester aliachia cheko ya chinichini ambayo ilinifanya niweke nadhiri moyoni mwangu kwamba nitamfunza adabu nikirudi nyumbani….
Mary : nimekueleewa usirudie Tena mi naumia umavyokua unanifanyia ivyo.
Nashukulu Mungu Mery alikuwa ni mwelewa na aliweza kunielewa basi nikamuaga na kuondoka zangu kwenda dukani kwangu,
Nikiwa na muwaza Mary njiani nilikutana na rafki angu wa kitambo Sana Eric ambae tulipoteana kitambo kirefu baada ya salamu nilimuachia namba zangu na kumwambia atanitafuta kwani kwa muda ule nlikua na wahi kufungua duka langu la bidhaa tofauti tofauti, kwa kweli nlichelewa na kukuta wateja wangu wananisubili pale dukani hivyo sikua na budi nliomba radhi nakuwa hudumia ilipo timia mida ya saa 9 nliona gari ikipaki mbele ya duka langu nlitoka njee ili nione vizuri……..
Na kweli sikuamini macho yangu nilichoona…..itaendelea
Je Clinton ameona nini na vipi kuusu mambo yake ya shule usikose muendelezo wa simulizi hii nzuri


No comments:

Powered by Blogger.