Breaking News
recent

MAPENZI SAFARI


 

Na Charles N Matagi

U hali gani mpenzi, mwenzio nakusalimia

peke angu siwezi, moyoni nta nagugumia

amini sina atamtetezi, ntabaki naugulia

Njooo basi mpenzi, na moyo uzidi tulia.



Alipanga mwenyezi, mimi kukuchagua

Walisema siwezi, penzi kulipigania

Walileta uchochezi, mbali tulitupilia

Sisi sasa ni wapenzi, na mbali tunaelekea.



Nakusifu laazizi, upendo unaonipatia

Kwa penzi lako sijiwezi, sitotoka nakuambia

Hakika unanienzi, sifa zote ninakupatia

Baki na mimi mpenzi, tuzidi kulifurahia.



Maneno yao si kitu, kama utanishikilia

Tena awata thubutu, kama utawapotezea

Kwani wabaya ni watu, usiwape pakuingilia

Achana nao mafyatu, safari izidi endelea.

No comments:

Powered by Blogger.