Breaking News
recent

LINZA WA MAMA

Ilipo ishia sehem ya kwanza : juma na Linza wanakubariana kutembeleana mara kwa mara mbali ya kuwa juma anaitaji Linza ahame anakoishi ahamie kwake basi mapenzi kati ya wawili hao yanaanza sasa endelea....
simulizi sehemu ya pili
  • Msimulizi : MAPENZI!!, ona sasa maisha ya mapenzi yanaanza kati ya Juma NA Linza, safari hiyo ya mapenzi ikaanza ili hali wote wakiendelea na masomo huku Linza akikaendeleza kale kamchezo kake ka kuwadanganya mama na baba yake kila walipo jaribu kumpigia, ni miezi miwili sasa Linza akiwa chuoni anakutana na mashoga zake Zubeda na Avijawa.


Zubeda : (kwa sauti yenye utani) mtoto wee umepotea maana huonekani

Linza : nipo tuu shosti si unajua mambo ya  chuo tena.

Avijawa : (kwa utani zaidi)chuo wapi  mama sema ndoa tu (wote wakacheka)

Linza: nyie nao kila tukionana ndoa kwani   ni yeye tu, niacheni  mie mtoto wa mama Linza mie.

Avijawa : Saa huelewi nini na wewe au ndo ndoa  imekukubali .

Linza : (kwa sauti  ya  upole) Yaani  nawaza  mwenzenu ujue  sio  unene  tu  pia  nna  mwezi  wa  

pili  sasa  naingia  sijaziona siku zangu mwenzanu......

Zubeda :  khaaa !  mwali  wetu  we  kwahiyo  unataka  kumzalia  Juma  ivo....??  mimba  hiyoo

Avijawa : (anadakia) eeh!  shoga  sa  Juma  atakupa  nini  eeeh!  mama  katoe  kweli  mwali  wetu  katoee.

Linza : (anataka kuongea anakatishwa) jamanii

Zubeda : Jamani  nini  mama  katoe  hiyo  itakuharibia mambo  katoe kwakwel  katoe .

Linza : Jamani ngoja  kwanza  nikapime  na  kuzungumza  na   Juma  kuhusu hilo,(Mhh  kama  ni  mimba  nimekwisha mie Linzaa woooooh) akasema kwa  sauti  ndogo,

  • Msimulizi: Juma anatoka chuoni akiwa ana furaha  na  kuingia  ndani ambako anakuta ukimya  umetawala  huku Linza akiwa amelala kitandani  kifudifudi,Juma  anamrukia   Linza  kitandani  na  kuanza  kumchezea  ili aamke.
Juma:  (akiwa ameshangaa kidogo) mbona  hauko sawa Mama

Linza (huku akigeuka ) amna  J  kuna  kitu  kinanisumbua  J  wangu  na  nashindwa  nisemejee

Juma : Linza  wangu  mimi  we sema tuu  wala  usijali ntaelewa  ,unajua  unanitisha  Mama

Linza : Babe sijaziona siku zangu

Juma : Una maanisha nini ?

Linza : Mbona umekua mkali J

Juma :  Hapana  sijaelewa

Linza :  Nilipo toka  chuo nilipita  hospitali nikapima na  nikaambiwa nina....(anasita)

Juma  : Nambie mamaa una nini?

Linza : J nina mimba ya mwezi mmoja (anaachia kilio kwa mbali)

Juma : Sasa  unalia nini Linza usilie Mama me nipo tayari kulea mimba  na wewe usijali  mama tuzae

Linza : Kweli  tuzae J

Juma : Yeah my tuzae

Je Linza atakubariana na Juma kuwa wazae? vipi kuusu wazazi wa Linza wakipata Taarifa hiyo hali ya kuwa mama na baba Linza wanategemea mengi kutoka kwa mtoto wao? usikose katika toleo lijalo hapo juma Tano ...
                     

No comments:

Powered by Blogger.