MAKALA KUHUSU MNYAMA FISI...
Fisi (hyenas) ni mnyama aishie
porini afananae kama mbwa lakini tofauti yao ni kwamba fisi wanaishi kifamilia
pia wana koo(hyaenidae) na utawagundua kwa mwendo kwani Miguu yake ya nyuma ni mifupi.
Watu hupenda kumuita fisi bwana afya waporini sababu ya tabia yake ya kula
mizoga hivyo kitendo hicho hutafsir
iwa kama kusafisha pori
Zipo aina nne za Fisi, ambazo ni:
Fisi madoa(spotted hyena) ni
moja ya aina za fisi ambao ni wawindaji wazuri
wanaweza kujitafutia kitoweo chao wenyewe sio tu kutegemea mizoga ambayo huachwa
na wanyama kama Simba na Chui, Fisi
madoa pia hula ndege, mijusi na wadudu na huwa na urefu wa
futi 4 - 5.9 au mita 1.2 – 1.8, urefu wa miguu ya mbele au mabega ni futi 2.5
hadi 2.6 au sentimita 77 hadi 81 na uzito wa kilo40 hadi 86.
Fisi wa kahawia(brown
hyena) ni wapili kwa uzito baada ya fisi madoa wakiwa na urefu wa sentimita 130
hadi 160 na uzito wa kilo34 hadi 72.6.
Fisi mwenye
mistari ya rangi mwilini (striped hyena), ana urefu wa sentimeta 100 hadi 115,
urefu wa miguu ya mbele ni sentimeta 66 hadi 75, mkia ukiwa na urefu wa
sentimeta 30 hadi 40
Aina ya
mwisho ni fisi aina ya Aardwolves (proteles cristata) kama ijulikanavyo
kisayansi. Fisi hawa ni wadogo kuliko aina nyingine tatu wakiwa na urefu wa
sentimeta 85 hadi 105 huku mikia yao ikiwa ni robo ya urefu wao na uzito wa
kilo 8 hadi 14.
Wanyama hawa wapo wa kutosha kwenye mbuga za ngorongoro, mikumi, Serengeti na pia bila
kusahau katavi, ni wanyama ambao kibali cha kumuweka kwenye bustani ya wanyama (
zoo) unaweza ukakipata ndani ya muda mfupi sana na ni maarufu kutokana na wingi
wao kuliko wanyama wawindaji na wala nyama wengine kama Simba na Chui. Wanyama
hawa hawachagui sehemu ya kuweka makazi yao ilimradi kuwe na chakula na maji,
sehemu hata kama ni kame, vichakani,
pori ndogo ndogo, hata sehemu ambazo zina ukijani sana mabwana hawa huweza kumudu kuishi na hivyo tuna weza sema
Fisi yeye popote kwake kambi hachagui wala habagui.
Kama
ijulikanavyo kwamba fisi hatulii sehemu moja mpaka awe amezeeka au anaumwa basi
ni hivyohivyo wakati wakujamiiana, wanyama hawa hutumia muda mchache sana
katika tendo hilo kwani mpaka fisi dume amalize kumpanda fisi jike ni dakika
tano (5) tu. Pia tabia nyingine yakustaajabisha kwa mnyama fisi ni kwamba Fisi
huanzisha uhusiano na fisi mwingine kutoka kwenye koo tofauti na yake na
huanzisha familia nae, baada ya mahusiano ya siku kadhaa yaani fisi kabla hajaoa
nae anapitia hatua ya uchumba.
Fisi hubeba
mimba kwa miezi mitatu na kama ikatokea amezidisha basi atazidisha siku chache
sana, huzaa watoto kuanzia wawili mpaka wanne ambapo jambo la kushangaza ni
watoto hao huzaliwa wakiwa macho yaani wanaona tofauti na wanyama wengine ambao
huchukua muda kufumbua macho na kuona. Watoto hao huanza kula nyama wakiwa na
umri wa miezi mitano ila hunyonyeshwa kwa muda wa miezi 12 hadi 18 na baada ya
miaka miwili mama yao huwafukuza kwani wanakuwa wamefikia umri wa kujitegemea.
Fisi huishi zaidi ya miaka20.
·
Moyo wake ni mara mbili ya moyo wa kawaida
wa mnyama.
·
Fisi madoa hula robo tatu(1/3) ya uzito
wake mwenyewe kwa mlo mmoja.
·
Fisi madoa anaweza kukimbia umbali
kufikia kilometa 60 kwa lisaa.
·
Watu husema fisi ni waoga lakini pia ni
hatari sana wakipata fursa ya kushambulia mnyama au binadamu kwani hawana
papara wakiwa wanashambulia.
·
Kati ya aina zote za fisi, fisi madoa na
wamistari ndio ambao wanajulikana sana kwa kushambulia na kula binadamu.
·
Fisi hujali sana watoto wake wakati
wowote kiasi kwamba huwatengea watoto wake chakula ambacho hakiguswi na fisi
yoyote na ukitaka kumchokoza yeye na Koo nzima basi mchokoze mwanaye.
·
Fisi huhusishwa na mambo ya kishirikina
sababu baadhi ya viungo vyake kutumika kutengenezea dawa za asili.
·
Fisi jike ni mkubwa na mwenye nguvu na
asie mvumilivu (mshari) kuliko fisi dume, hii ni kwasababu fisi jike wana mara tatu
ya tezi ya testosterone kwenye miili yao kuliko dume na hupelekea wao kuwa
viongozi wa koo zao.
TABIA MBALI MBALI ZA
MNYAMA FISI;
·
Fisi anauwezo mkubwa mno wakunusa na
kuhisi umbali mrefu hivyo hutambua kama kuna chakula (mizoga), maji, wadudu au
mawindo yapo wapi. Mfano kujua ni nyumbu yupi mzembe kwenye kundi la nyumbu.
·
Ni wanyama wenye pirika nyingi kuliko
wanyama wengine hivyo kutulia sehemu moja kwao ni mwiko.
·
Fisi ni wanyama wenye umoja na
ushirikiano sana kwani ukichokoza mmoja ni sawa na kuchokoza ukoo mzima kwani
huitana sehemu husika kwa sauti mbalimbali kuashiria kuna hatari.
·
Fisi ni mnyama ambae haamini katika
kushindwa katika ugomvi hivyo wakiwa wanapigana lazima mmoja afe au akimbie
akaite wenzie.
·
Ni marufuku kwa fisi wakati wa kula
kujipakaza damu usoni kwani wenzao humuona mlafi hivyo humgeuza yeye kitoweo.
Wanayama hawa hujitahidi sana kuzingatia usafi wakati wa kula na baada, hata skama
akijipaka damu basi ni lazima ajirambe mpaka ziishe kabla hajamaliza kula.
·
Wahisipo harufu ya damu popote pale basi
mzuka wao huongezeka maradufu kuliko mwanzo.
·
Fisi humuogopa sana simba dume kuliko
jike hivyo wakimkuta jike akiwa na kitoweo humchokoza na kumsumbua ili kumpora
nyama lakini akiwepo tu simba dume hukaa mbali na wao mpaka wamalizapo kula ili
wakale mifupa.
·
Fisi hutoa sauti mbalimbali kama njia ya
kuwasiliana na sauti hizo hutofautiana kutokana na tukio husika. Mfano hucheka
sana wakati wanakula mpaka wanamaliza kuonyesha wanafurahia mlo wao, hivyo
huwasaidia sana kuwapumbaza wanyama wengine wasiwasogelee wakati wakula.
No comments:
Post a Comment