Breaking News
recent

LEO NI SIKU YAKO KIJANA KAMILISHA NDOTO ZAKO..


Leo ni siku yako kijana.
Na Charles N Matagi
Naangalia kesho, kesho yako kijana
Nayaona mateso, kama autopambana
Utashindwa inua uso, kwawale wanaokutazama
Leo ni siku yako, unapaswa kupambana

Miaka mingi shuleni, mpaka chuoni ukazama
Mbona aupo kileleni, jahazi lako linazama
Mpaka tunasahau dhumuni, la wewe kwenda kusoma
Leo ni siku yako, unapaswa kukomaa

Shule ufati ajira, acha zako lawama
Unapewa tu dira, ya kuweza kusimama
Basi fanya himahima, kablan ya jua kuzama
Leo ni siku yako, timiza ndoto zako

Zama zimebadilika, kaka shtuka
Usitandike mkeka, anza kufanya hekaheka
Utatoboa haklika, siku yako imefika
Leo ni siku yako, okoa kizazi chako

Futa machozi yako, kaza mkwiji wako
Ongea na nia yako, tumia na nguvu zako
Ukane udhaifu wako, dhiilisha uhodari wako
Leo ni siku yako, kamilisha ndoto zako

Tumia elimu yako, kusaidia wazee wako
waliwekeza kwako, uwaondolee sikitiko
Tumia ujuzi wako, kusaidia jamii yako
Kwani leo ni siku yako, pigania muda wako

No comments:

Powered by Blogger.