MITANDAO YA KIJAMII NA MAISHA YA VIJANA
Na Denis N Nguno
Tangu
mwaka 2006 mitandao ya kijamii imekua kwa kasi Sana hasa katika nchi za
kiafrika. Kuna mitandao mingi sana ya kijamii mfano; facebook, Twitter,
Instagram, 2go na mingine mingi.
Maisha
ya vijana wengi kwa sasa yapo katika mitandao ya kijamii, sijui ni wangapi
watakubaliana nami kwamba kijana wa sasa yupo tayari kumiliki simu janja(Smart
Phone) ya laki 8 na nusu ili tu aweze kuwa na account ya instagram hela ambayo angetumia kama mtaji na kuanzisha biashara.
Kila
kitu kina faida na hasara, hivyo maisha ya vijana kuwa kwenye mitandao ya
kijamii kuna faida na hasara zake
Zifuatazo
ni baaadhi ya faida za maisha ya vijana kuwa kwenye mitandao ya kijamii,
- Kwa kijana mwenye uwezo wa kufikiria anaweza kujifunza kupitia kwa vijana waliofanikiwa kwa kupitia mitandao ya kijamii, kuna vijana wengi waliofanikiwa na maisha yao yanaonekana kupitia mitandao ya kijamii mfano mzuri ni Diamond Platnumz, vijana wengi wanaweza kujifunza kupitia yeye na kujikwamua kiuchumi kupitia maisha yake.
- Upatikanaji wa elimu kwa njia ya mitandao ya kijamii, mfano kijana anaweza kujifunza ufundi mbali mbali kwa kupitia mitandao ya kijamii kwa kuona, kusoma na kusikiliza hivyo ni rahisi kwa kijana wa daraja lolote la elimu kuendelea kujifunza.
- Kukua kwa mahusiano na kujenga umoja kwa vijana, mitandao ya kijamii inaweza sababisha kukua kwa mahusiano kwa vijana, mfano mtu wa Mwanza anaweza kufahamiana na mtu wa kigoma kwa kupitia (Instagram) moja kati ya mitandao pendwa ya kijamii. Hivyo kupitia mitandao ya kijamii vijana wengi hufahamiana na kujenga umoja kati yao.
- Pia biashara zinakua Kwa kasi kupitia mitandao ya kijamii kwa vijana wengi kwa hutangaza biashara zao kwenye mitandao ya kijamii, jambo ambalo huwaongezea kipato na kuwasaidia kukuza biashara zao.
Mbali Na
hizo faida zitokanazo na maisha ya vijana kuwa mitandaoni pia kuna hasara
wanazozipata vijana na jamii kwa uwepo wa mitandao ya kijamii, na zifuatazo ni
baadhi ya hasara za maisha yao kuwa katika mitandao ya kijamii;
- Vijana wengi huishi maisha ya kuigiza kwenye mitandao ya kijamii, vijana huwaiga maisha watu maarufu hivyo husababisha wao kujiumiza kiuchumi kwa kutaka tu kuwa sawa na mtu fulani jambo ambalo hupoteza dira kwa vijana wengi.
- Kuongezeka kwa wizi na utapeli, vijana wengi hudhulimiwa kwa njia za mitandao, mfano kijana anaweza kuagiza kitu alichokiona mtandaoni lakini pindi kinapo mfikia kitu hicho cha weza kuwa sicho au ndicho lakini feki.
- Mitandao ya kijamii husababisha kuto kuaminiana baina ya wapenzi na kusababisha kuvunjika kwa mahusiano,siku hizi hata ujumbe mfupi(message) au komenti tu husababisha kuvunjika kwa mahusian, pia ni rahisi kupata (mbadala wa ulie nae)mchepuko hivyo mitandao ya kijamii huvunja mahusiano ya vijana wengi.
Maisha ya vijana kwenye mitandao ya kijamii kusababisha kushuka kwa kipato cha vijana kwani hata kidogo wanachokipata wanakitumia kwa anasa mfano kijana anaweza akanunua nguo ya gharama, ili tu aweze kuonesha kwenye mitandao ya kijamii, hivyo mwisho wa siku vijana wengi hujikuta hawana kipato chochote na hivyo kuongeza umasikini katika jamii. Hatuna budi vijana kufanya kazi na kujiwekeza kwa dhati katika kupigania fursa zinazo tokea kutokana na mitandao na kuacha na kufatilia yale ambayo ayana matokeo chanya kwenye maisha yetu. Weka simu kando fanya kazi kwa uhakika.
No comments:
Post a Comment