HAPA KWANGU MARUFUKU.
Mimi hapa ni mzima, hofu kwenu watanzania
Leo hii nna ujumbe, nataka kuwafikishia
Mnitunze
mnilinde, mimi nawategemea.
Mlinilea
vyema, hapo zamani nawambia
Mlinilinda
vyema, hili nna wathibitishia
Sasa
shida ipo wapi, mbona mnani mendea
Mimi
ni mtoto wenu, sasa nawa kumbushia
Baba
na kaka zangu, sikieni kilio changu
Moyo
nina machungu, siwezi muachia Mungu
Mnanifata
kwa mafungu, eti mnataka hisia zangu
Mnanipa
kizungu zungu, mnavyoniona zuzu.
Mbali
na nguo zenu nadhifu, natabia zenu sumbufu
Kwa
ujinga wenu na hofu, Mnaendeleza uchafu
Imani
zenu potofu, na akilizenu dhoofu
Msijifanye fukufuku, hapa kwangu marufuku
No comments:
Post a Comment