NJIA AMBAZO UNAWEZA TUMIA KUPATA MPENZI AMBAE NI SAHIHI WAKUKUFAA KATIKA MAISHA
Na Charles N Matagi
Maisha ya
mapenzi ni safari ndefu ambayo ili ianze ni lazima watu wawili waingiao kwenye
safari hiyo wote wawili kwapamoja wawe tayari na wawe wamejipanga kufanya ivo.
Je ni njia zipi zinazo weza kumsaidia mwanaume au mwanamke ambae ametoka kwenye
mahusiano na kuachana na mpenzi wake wa mwanzo kupata mpenzi mpya ambae
watadumu wote kwa mda mrefu au mpaka ndoa? Kwahiyo kuna mambo ambayo yanaweza kukusaidia
kupata mwanamke sahihi na atakae kaa na kuishi nawewe maisha ya furaha na amani
na hizi hapa ni miongoni mwa mbinu ambazo unaweza fanya kumpata mwanamke huyo
au mwanaume huyo…..- Jitahidi au hakikisha unampata mwanamke au mwanaume ambae ni rafiki yako au anaelewa mengi kuhusu wewe na maisha yako, yaani inamaana kabla hujamkubali mtu kama mpenzi ni vizuri zaidi kuwa na mtu unaemtarajia kuwa atakua wako katika mahusiano ya urafiki kwani itawapa mda mzuri wa kujuana vizuri na kufahamiana kiasi kwamba itawapa urahisi ata mkianzisha mahusiano mtakua mnajuana na mmezoeana kiasi kwamba kila mtu anakua huru kumwambia mwenzi wake mambo yote bila kuhofia, hiyo ni kwasababu tu mnajuana hivyo mahusiano yenu yatadumu japo sio kwa wote ila kama kweli katika wakati wa mahusiano kila mtu alikua anaishi maisha yake asili basi wengi huwa wanafanikiwa katika njia hii.
- Kuwa muwazi kwa mtu unaetaka kuanza nae mahusiano, hili ni suala dogo lakini linawashinda wengi na linawafanya wengi washindwe kudumu katika mahusiano punde tu wanapo kuwa wameanzisha mahusiano hayo, uwazi ni neno la kawaida kulisikia maskioni mwetu ila linamaana kubwa sana katika maisha yetu ya mahusiano na ndoa kwani kama mmoja kati ya watu waliokwenye mahusiano atagundua mwenzie amemficha kitu basi atapoteza ile hali ya kujiamini katika mahusiano. Ila hili sio lengo langu kwaleo, kwaleo nazungumzia wale wanaotaka kuanzisha mahusiano inatakiwa umwambie ukwel kuhusu wewe mwenyewe yaani tabia na aina yako ya maisha unayohishi na ulikotoka yaani umwambie ni nini kilimshinda yule ulieachana nae au aliekuacha hii itamfanya unaetaka kuanzisha nae mahusiano kujua ni mtu wa aina gani anaetaka kuwa nae na kama atajua kabisa hawezi kukusaidia kwa tabia au mambo yako uliyo mwambia basi atakua wazi kukwambia na hili litakusaidia wewe kupata mda wakumtafuta mwingine bila kuumizwa na kuachwa tena .
- Mfanye ajue malengo yako na ni nini unataka yeye akusaidie katika maisha yako,kwa wale wakristo tukisoma Mwanzo sura ya pili mstari wa kumi na nane “Bwana Mungu akasema Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye”. Tunaona ni lazma mtu uwe na malengo yakufika sehemu flani na hili ufanikiwe ni muhimu kuwa na msaidizi ivo ukiwa unataka kumtafuta mtu ambae unataka kufanya nae maisha ya mahusiano ni muhimu ajue malengo yako ili aone je nayeye anamalengo yakufanana nawewe au La! Hili litakusaidia wewe kupata mwanaume au mwanamke ambae mtafika nae mbali katika maisha ya mahusiano au ndoa.
- Hakikisha unatumia moyo kuchagua na si macho,watu wengi sikuizi tunashindwa kutofautisha kati ya chaguo la moyo na chaguo la macho? tupo kwenye mahusiano kwa sababu moyo umechagua au macho yametaka uwe nae basi ili kupata mwanamke au mwanaume ambae ni sahihi kwako ni muhimu kujua ni kipi kime chagua kama ni macho basi ujue ni njia gani unaweza ifanya ili kuuridhisha moyo kuwa umechagua kitu sahihi na kama ni moyo basi hivyo hivyo fanya kushawishi macho kwa maelezo yakina kuhusu mahusiano ya moyo na macho basi tukutane katika somo lijalo.
Hayo ni machache
kati yamengi ambayo mtu anaweza kutumia kama njia za kumpata mpenzi mpya ambae
wataishi kwa muda mrefu na kwa amani.
(chanzo cha picha mtandaoni)
No comments:
Post a Comment