MJUE MNYAMA TEMBO NA TABIA ZAKE
TEMBO (ELEPHANT)
Mbali
na uzuri na humuhimu wa wanyama hawa ila takribani Tembo 100 uuwawa na
majangiri kwaajiri ya pembe zao.
JINA LA KISAYANSI : LOXODANTA AFRICANA
Tembo
au Ndovu kwa Kiswahili, kwa kingereza anaitwa Elephant pia kwa jina la
kisayansi anaitwa Loxodanta Africana. Tembo ni mamalia mkubwa kuliko wote ambao
wanapatikana ardhini Huku inaelezwa kuwa Tembo dume huweza kufikia uzito wa
kilo kuanzia 2000 – 6000 ambayo ni sawa na tani 2 – tani 6 na kuendelea na Tembo
jike yeye ana kilo 2000 – 4000 ni sawa na tani 2 – 4. Tembo anaurefu wa hadi
futi 13.
- Tembo huishi miaka 60 – 65, Tembo kama wanyama wengine wasiokula nyama Tembo huwa anakula nyasi, mizizi, magome ya miti pamoja na matunda na Tembo ili ashibe anahitaji kula kuanzia kilo 250 – 300 kwa siku na maji lita 160- 200. Mbali na ukubwa wa mwili wao tembo anatembea bila kusikia kishindo kabisa kwani miguu yake inaulaini kama sponchi kitu ambacho kinamfanya anakua miongoni mwa wanyama atari katika kushambulia. Tembo anaogopa nyuki kuliko kitu chochote na pia hapendi kelele.
- Kuna spishi mbili za tembo, ya kwanza ni tembo wa Afrika na ya pili ni Tembo Asia na katika tendo la ndoa Tembo hutumia masaa 12 kukamilisha mzunguko mmoja,huku wakitumia masaa sita (6) kuandaana na sita (6) yanayofuata ni kwaajiri ya tendo lenyewe. Uume wa tembo unakadiliwa kuwa na kilogramu 27 ambapo ukifanikiwa kuuona kwa nyuma unaweza ukadhani ni mguu wa tatu na wakati huo huo tembo dume huejaculate lita 5 kwa tendo 1.
- Wakati binadamu akiwa anabeba mimba kwa miezi tisa, katika suhara la uzazi Tembo yeye hubeba mimba miezi ishirini na nne (24) ikiwa ni sawa na miaka miwili na hiyo inamfanya hawe ni mnyama anaebeba mimba muda mrefu zaidi ya wanyama wote ambao wameshatambulika duniani na pia hujifungua mtoto mmoja tu akiwa na kilo 80 hadi 120. Tembo ananyonyesha takribani miezi 22 na huwa inachukuwa miezi 16 mpaka meno yao kuanza kuota, meno yao huonekana zaidi akitimiza miezi 30 tangu kuzaliwa. Tembo jike hubeba mimba kila baada ya miaka miwili.
- Tembo hutumia pua na masikio yao kwaajili ya mawasiliano yao na kujua ishara mbalimbali kama hatari, kwa kutumia maskio yake Tembo anaweza kusikia umbali wa kilomita nane(8) mbali na hilo Tembo wa Afrika inasadikika ndio mnyama mwenye hisia nzuri kuliko mnyama mwingine yoyote pia tembo ni miongoni mwa wanyama wenye kumbukumbu nzuri. Katika masuala ya familia Tembo dume mmoja anakuwa anamiliki majike wawili mpaka wanne huku uongozi wa familia ya tembo unakua chini ya Tembo jike ambae huwa ndio kiongozi wa kundi lote la Tembo(martinia society). Mbali na sifa zingine za mnyama huyu pia ndio mnyama pekee anapitisha maji puani kwanza kisha mdomoni kisha kooni, Tembo ulala masaa mawili mpaka matatu kwa siku.
- Tembo pia ni mnyama muhimu mbugani kwani kwa uwepo wake kipindi chakiangazi Tembo utumia meno yao kuchimba maji ardhini hivyo uwawezesha kudumu kwenye mazingira kame na maji hayo pia uwanufaisha wanyama wengine kwa matumizi yao, kwa kutumia miili yao na mkonga uwawezesha kukata miti na matawi kwaajiri ya chakula ambacho pia na wanyama wengine utumia, kulingana na miili yao mikubwa pia utengeneza njia katika misitu minene, aidha Tembo ni chanzo kikubwa cha kuongeza na kuamisha mimea mbali mbali kutoka kwa watu kwenda polini au poline kuja kwenye mazingira ya watu kwa kutumia kinyesi chake ambacho kimetokana na ulaji wake wa mimea yenye mchanganyiko na mbegu, kokote wanako ishi Tembo wanakawaida ya kuacha kinyesi kilicho jaa mbegu ambazo uchipua na kuwa miti au misitu mbayo uja kuwa ni chakula kwa wanyama wengine. Mbali na kinyesi chake kutumika kama dawa ya asili ya binadamu pia kinyesi chake utumika kama chakula kwa wanyama kama Tumbili, ndege na nyani.
picha na Insect Safaris Adventures |
KUMBUKA:
Kama tulivyosema tembo anakumbukumbu na anajua hatari kwa haraka zaidi inashauriwa ukiwa mbugani na ukataka kumpiga picha
tembo inashauriwa kuzima flash light kwani akiiona anaweza kuwadhuru. Tanzania
tembo hupatikana kwa wingi zaidi katika mbuga za Tarangire, Ngorongoro,
Serengeti, Ruwaa na Mikumi.
{picha zote chanzo ni mtandaoni}
MAKALA NA CHARLES N MATAGI
No comments:
Post a Comment