TENDO NALIFURAHIA (shairi)
TENDO NALIFURAHIA
Charles N Matagi
Sogea
karibu yangu uaridi, uniponyae kwenye baridi
mpenzi
nifukize na Udi, mimi ni wako jitahidi
Ntaongeza
zangu juhudi, kukung’ang’ania sina budi
Nishike
shike mpenzi, tuwakomeshe walanguzi
Kwako
sikupotea njia, mmoja moyoni umeingia
Nakusihi
mpenzi tulia, penzi lako pigania
Hakika
akuna wakukutoa, jitahidi sikilia
Shika
shika nakwambia, wabaki wanaumia
Tendo
nalifurahia, ujuzi umejariwa
yote
unaponiachia, mwanzio nachanganyikiwa
tamu
unapoibugia, waluwalu ninakuwa
nipe
nipe mapenzi, wajiweke kitanzi
kwa
utamu wako laazizi, mbali sito sogea
nitazidi
kuwa wako mpenzi, utamu uzidi kolea
amini
mi ni wako nienzi, mpenzi umeniwezea
hii
ni hadithi yako mpenzi, nikupendae nakuhadithia.
No comments:
Post a Comment