Breaking News
recent

KAPUNI (Simulizi ya kusisimua)

Image result for africa traditional basketKAPUNI

·       Sehemu ya kwanza

Akiwa hospitali... OMARI: ( mapema, nakumbuka Baba hakutaka kuacha kunionesha njia kwani alinambia mwanangu katika maisha sisi wanaume tunapitia changamoto nyingi sana lakini simba wangu usikate tamaa kubali kupambana na ukatae kushindwa, na wanawake tia KAPUNI  "mwanangu dunia hadaa ulimwengu shujaa, usipaparikiie maisha kwani dunia ya leo tayari imevaa kofia ya moto, cheza michezo yote lakini mchezo mmoja tu usiucheze, nao ni kujisahau, katika maisha vijana wengi wanajisahau, ndiyo maana wengi wanapotea na kuzikwa bila kujua. Mwanangu sisi wazazi wako tumezeeka sasa lakini matumaini yetu ni wewe, elimu ni ufunguo wa maisha soma mtoto wetu uje uyafungue maisha yetu haya, kamwe usiiendekeze tamaa kwani tamaa ikiwa mbele mauti huwa yako nyuma. Mwanangu ukiona nyani kazeeka ujue kakwepa mishele isiyo ya kuhesabika, sisi tumezeeka lakini wewe ndiyo mkombozi wetu, SOMA MTOTO WETU". laiti ningejua nisinge yapuuzia maneno ya Baba. nakumbuka mama hakuwa nyuma nae aliniambia mwanangu ukilima Leo usilazimishe uvune kesho kwani subira siku zote huivuta heri." Lakini yote haya yamekuwa kama makelele kwangu, ona sasa dunia imenikumbusha yote haya, inaniuma sana, inauma, inauma, kweli !, ushupavu na uhodari wangu aliokuwa ananisifia mama uko wapi sasa!?, uzuri wangu na marafiki zangu wako wapi sasa!? Hakika nimeumbuka, hakika dunia imenifunza, ndoto zangu zimeyeyuka kama barufu juani, malengo yangu sasa KAPUNI nimefunzwa kulima mti wa matunda lakini nmelima mti wa miba sasa navuna miiba mikali inayouchoma moyo na mwili wangu. Nipo hapa kitandani,  Hata nishasahau nani alinileta hapa ndani, nimeongezewa maji na damu hadi mitungi imenizoea, kitanda hiki nakiona sasa kama ndiyo umbo la kaburi langu kwani kupona kama ingekuwa ni Leo au kesho ningejivunia sana lakini kwa sasa hata tone la matumaini sina, muda wowote nitaiaga dunia tayari kwenda ardhini kutengeneza madini, Omari mtoto wa Ridhiwani mtoto  niliyeitwa simba sasa hata kuitwa sungura sifai, mwili sasa umekonda, mabega yanakikimbilia kichwa kwa kasi ya ajabu, kwani nilikuwa tayari nimeshawasahau wazazi wangu lakini imenikumbusha kwa kunichapa viboko vya magonjwa,mawazo na matatizo. Mbona safari yangu ya elimu nilianza vizuri tu!?, kwanini nifike huku chuo niishie njiani?).
Nakumbuka miaka kadhaa iliyopita..........
RIDHIWANI (Baba omari}; mwanangu nimefurahi sana kusikia umeongoza mtihani wa darasa la nne, hakika wewe ndiyo mkombozi wa familia hii.
OMARI; (huku tabasamu likinitoka kwa furaha), Asante pia baba na nakuahidi kusoma kwa bidii hadi nifikie malengo yangu na kukuokeni nyinyi wazazi wangu.
BABA OMARI; mwanangu, ni heri Mimi nivae nguo zilizo chakaa, tulale njaa Mimi na mama yako lakini wewe lazima usome.
OMARI; nakushukuru sana baba yangu, ipo siku mtafurahi na kuishi maisha mnayoyatarajia kutoka kwangu.
KITANDANI; (hakika nilipokuwa  nasikia hayo maneno moyo wangu ulikuwa unajawa na machungu sana, hata kama  nikiwa nimelala, nilitamani niamke niendelee kujisomea kwani sikuona mhimu wa Mimi kulala huku wazazi wangu hawalali usiku kucha wanawaza jinsi ya kunisaidia kufikia malengo yangu na siku moja nije niwasaidie. naikumbuka vizuri sana siku ambayo baba yangu alitoa machozi ya furaha kwa sababu yangu.)

BABA OMARI; Daniel nasikia matokeo ya darasa la saba yametoka, namtafuta mwalimu  lyakurwa  nimuulize umepataje.
OMARI; hata Mimi nimesikia lakini sijajua nimepata ngapi na hapa nilipo nateteka mwili mzima.
mara paap! sijamaliza kuongea simu ya baba inaita
BABA OMARI ; (anaongea na simu), haloo!!!
SAUTI; haloo! Naongea na mzazi wa OMARI RIDHIWANI?
BABA OMARI; ndiyo mimi.
SAUTI; samahini Mimi ni mwalimu taaluma katika shule ya msingi majengo naitwa mwalimu Msuya,  napenda kuwapa Hongera wewe na mtoto wako.
BABA OMARI; (Huku moyo ukimdunda haraka na kwa nguvu), Hongera ya nini tena mwalimu?
SAUTI; mtoto wako Daniel amefaulu mtihani wa darasa la saba, shule inakupa pongezi kwa sabab ndiyo mwanafunzi pekee aliyefaulu kwa ufaulu mkubwa,  na amelitangaza jina la shule. Hongera sana.
BABA OMARI; (mithili kutupa simu na kuanza kushangilia,), hakika mungu hamtupi mja wake, Leo hii Omari mwanagu unafaulu na kuniletea sifa Mimi baba yako, (huku machozi yakimtoka kwa furaha), Omari sijuti Mimi kulala njaa kwa sababu yako kwani matunda yako nimeyaona, Hongera sana mwanangu, Hongera sana, natamani nikupe zawadi ya kipekee lakini uwezo sina.
OMARI; baba Asante sana, najua bila wewe nisingekuwa hapa leo, ushauri wako Huduma yako vyote vimechangia Mimi kufaulu, nakushukuru sana baba, baba naomba nikuahidi kuwa kama nikifanikiwa siwezi kuwasahau wazazi wangu, nitasoma kwa bidii zote na kuhakikisha naikoa familia yangu.......!

KITANDANI; (Ndipo pilika pilika za kujiandaa zilishamili ili Mimi niende shule, nakumbuka baba alifanya kazi kama mtumwa, iwe asubuhi Iwe jioni mzee Ridhiwani alikuwa ni yeye na vibarua ili tu mwanae niweze kuingia shule ya sekondari, sikumtupa mkono kazi zingine nilifanya naye huku mama naye akitusaidia, kila mtu aliongea mengi juu ya wazazi wangu, Hata kuna wakati majirani walicheka na kuwashangaa wazazi wangu, lakini mama na baba hawakukata tamaa huku wakiamini na kujipa moyo kuwa IPO SIKU wataheshimiwa, hakika nimewakosea sana wazazi wangu, nimewaangusha na kamwe siwezi kuwainua, Yale matumaini yao yamegeuka na kuwa maumivu na majuto. Kwanini mungu ameruhusu Mimi niwe hivi?, muda uliwadia wa Mimi kuondoka nyumbani na kuielekea shule niliyochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza, hasira zile zile nilikuwa nazo, kusoma bila kukoma, baba na mama maombi yao yalifanya kazi kwani nilifika salama mkoani mwanza, na nikaendelea na masomo ya kidato cha kwanza.)
 Mwalimu Hassani; asante sana mwalimu mkuu kwa kunipa nafasi hii, kwanza kabisa napenda kuwakaribisha wanafunzi wote wa kidato cha kwanza katika shule yetu, hakika mko sehemu sahihi jisikieni mko nyumbani. Pamoja na kuwakaribisha ningependa kuwashauri kwamba, katika shule yetu hatukubali watu wenye tabia mbaya na ufaulu wako  ndiyo utakusaidia kuvuka darasa moja kwenda darasa jingine……………..hakika nayakumbuka maneno haya kwani ndiyo yalikuwa chachu ya kufaulu katika  masomo yangu, katika kipindi hiki nilipata marafiki wengi sana wakiume pamoja na wakike, pengine jitihada na mafanikio yangu yaliwavuta wengi na kuwafanya watamani kuwa karibu na mimi.
OMARI; kama mwalimu alivyoelekeza, Lugha ni sauti za nasibu zenye kubeba maana na zilizokubaliwa na jamii fulani
MARRY; Nini maana ya sauti za nasibu?
OMARI; Sauti za nasibu ni sauti za kubahatisha. maana zilitokea kwa bahati tu kwa binadamu.... mbali na kua na maana ya kawaida pia kuna lugha ya ishara inayotumiwa na bubu. pia katika fani ya programu za kompyuts ni kawaida kuongea juu ya " lugha ya kompyuta"
MARRY;hapo sawa nimekuelewa ommy.
OMARl; haya tutaendelea badae marry.
MARRY;haya haina tatizo lakini naomba tukanywe chai kabla haujaenda ommy.
OMARI; mmmmh! Hapa sina hata mia mdogo wangu wewe nenda tu.
MARRY; kuhusu hela wala usijali kaka yangu.
OMARI; una maana gani?
MARRY; twende nitakulipia.

KITANDANI; japokuwa mara nyingi niliiishi bila hela lakini maisha yangu yalikuwa ya furaha kwa sababu kila mwanafunzi alikuwa ananipenda na kunisaidia pale nilipokwama, hakika japokuwa wazazi wangu walikuwa masikini laikini mimi nilikuwa kama mtoto wa tajiri, kwani kuna wakati hata sikuenda nyumbani muda wa likizo kwani marafiki zangu wengi walikaribisha kwao.
VICENT; hivi ommy likizo hii unaenda wapi?
OMARI;dah! Ndugu yangu hapa nawaza sana maana nimeongea na baba kasema hana hela ya kunitumia ningeenda nyumbani. nahisi nitabaki tu shuleni
VICENT; dah lakini usijali kaka, mimi naona ni bora tungeenda kwetu.
OMARI; hapo utakuwa umenisadia sana rafiki yangu.
VICENT; haina shida, unaweza kumpigia baba asisumbuke sana.


KITANDANI; ni kidato cha nne sasa, maisha yangu ni kitabu na kalamu, hukuwahi kuniona nimekaa bila daftari au kitabu, hakika nilikuwa mwanafunzi mfano katika shule hiyo, mtoto wa masikini mimi sikubweteka na sifa walimu walizonipa, lakini nilizitumia kama chanzo cha mimi kujitahidi katika masomo yangu, zawadi nyingi nilikuwa tayari nishapokea kipindi hiki ikiwemo zawadi ya elfu hamsini kutoka kwa mkuu wa shule baada ya kuwa mwanafunzi bora katika kidato cha pili na zingine nyingi sana, kalamu niliyoitumia kuitandika elimu ipasavyo lakini kalamu hii hii naitumia kuandika ujinga nilio ufanya kwa wazazi wangu…………. Hakika sikuzani kama nitaishia njiani katika masomo yangu inaniuma sana lakini maumivu yangu sidhani kama yatafikia ya wazazi wangu siku watakapo pata taarifa hizi.


NAAMU HUU NDIYO MWISHO WA SEHEMU YA KWANZA, TWENDE PAMOJA KATIKA SEHEMU INAYOFUATIA NAMBA KWA WANAOHITAJI NI 0759592804 WHATSAAP


thanks to ma young brow NOURISH
          to ma blood Mr ROMANTIC
KEEP IN TOUCH AT YOUR STUDY

No comments:

Powered by Blogger.