Breaking News
recent

HATUA ZA MSINGI KUZINGATIA KABLA YA KUFANYA MAAMUZI

Image result for power of disetion

            Ilikufanya maamuzi yaliyo sahihi katika maisha nilazima  uzingatie muda sahihi wa kufanya maamuzi hayo. Hivyo: hivi ni baadhi ya vitu vinavyoweza kukusaidia kufanya maamuzi hayo:
  1. Kwanza kabisa usifanye maamuzi ukiwa na furaha sana au ukiwa na hasira sana,  maamuzi utakayofanya ukiwa katika moja ya hali hizo mbili hapo (hasira au furaha kupitiliza) yatakufanya ujute hapo baadae
  2. Fanya maamuzi ya kweli bila kujali nani ataumia au nani hatoumia, kama kweli unataka kufanya maamuzi sahihi  basi chagua ukweli kwani maamuzi hayo yatakufanya uwe huru huko mbeleni na upunguza majuto
  3. Kamwe usitafute visingizio kubeba maamuzi yako. Kama kweli umenuia kufanya maamuzi sahihi basi chagua maamuzi ambayo yapo wazi usichague maamuzi ambayo yatakulazimu kutafuta visingizio ili kubeba maamuzi yako kuwa ni sahihi.
  4. Fanya maamuzi mara baada ya kufikiria na kufanya tafakari ya kina juu ya jambo unalotaka kulifanyia maamuzi, kwa njia hii itakupa uhakika juu ya lile unaloliamua kwani utakua unalijua vyema baaada ya kulifanyia tafakari pana
  5. Jua wazi maamuzi sahihi ni magumu sana na mara nyingi hupingwa, hivyo jiweke tayari kupambana na kusimamia maamuzi yako vilivyo.

No comments:

Powered by Blogger.