Achana na wizi fanya kazi
Na Charles N Charles
Za mwizi ni siku zako, angalia uwendako
Pambana na hali yako, usilete
chokochoko
Tumia nguvu zako, kushibisha
tumbo lako
Wizi si kazi kwako, utakuletea
sikitiko
maisha ni changamoto, yaliyo jaa
michosho
Yanachoma kama moto, ila punguza
utoto
Usiendekeze utoto, kijana
utachomwa moto
Wizi si kazi kwako, utakuletea
sikitiko
Mama Mima analia , jana alivamiwa
Hawafu amechukia, njiani ali ibiwa
Wanakijiji wameamua, wamechoka
kuibiwa
Wizi si kazi kwako, utakuletea
sikitiko
Juma amejitolea, kokote
kukufatilia
Nawengine wameingia, kundi kubwa
limekuwa
Kijiji chote chazizima, ulinzi
shilikishi ndio njia
Wizi si kazi kwako, utakuletea
sikitiko
Acha tabia ya wizi, ng’oa na hiyo
mizizi
Usije kuwa jambazi, nyumbani
ukaleta majonzi
autokuwa na mtetezi, watakapo
kuwekea kitanzi
wizi si kazi kwako, utakuletea
simanzi.
Kama unaweza shairi pia tuandikie na tuma kwenda watsap 0656109278
barua pepe nelsoncharlesmatagi@gmail.com
No comments:
Post a Comment