KWANINI WATU WANAUMIA NA KUTESEKA NA MAPENZI.
Kuumia na kuteseka huku sababu kubwa hikiwa ni mapenzi ni kitu ambacho kinamkuta kila binadamu huku kila mtu kikimkuta kwa wakati wake, kwa maana hiyo basi maumivu ya mapenzi huwa ayachagui wewe ni mdogo sana au mkubwa sana yakija yanakuja na utapata kuyasikilizia na kila mtu anaumia kwa aina na namna yake kwani kila utakae muuliza atakujibu kulingana na yeye alivyoguswa na maumivu hayo. Tuje tuone ni kwanini sasa watu wengi tunaumia na kuteseka na mapenzi,hizi ni sababu chache kati ya nyingi ambazo uwafanya watu wengi kuumia na mapenzi.
- Kuishi kwa mazoea, watu wengi tuliopo kwenye mahusiano ya kimapenzi tunajikuta tunaumia kwa kuachwa na wale tunaowapenda tu nikwasababu tulikaanao na kuishi nao kwa mazoea, nisikufiche mapenzi yanaitaji ubunifu na mbinu za mala kwa mala ili kufanya penzi kusimama kwani atakwenye upandaji wa maua nguvu ya kumwagilia unayoitumia kupanda mbegu ya Ua ndio inabidi hiwe mala mbili ya nguvu unayotakiwa itumia kumwagilia hilo Ua kuhakikisha alisinyai ni sawa na mapenzi yale uliyokua unafanya wakati wa mwanzo wa mahusiano inabidi uzidishe na sio kupunguza baada ya kuingia kwenye mahusiano kwa maana hiyo basi ili kuweza kukwepana na maumivu ya kuachwa basi ni lazima uishiuku ukimuona mwenzi wako mpya na kuamini anaitaji vitu vipya mala dufu zaidi ya hapo awali achakuishi kwa mazoea
- Kutokua muwazi na kueleza ukweli, wengi wetu tuliachwa au bado tunaachwa kwa sababu ya kuficha baadhi ya mambo ya msingi ambayo tunatakiwa kuwa shilikisha wenza wetu na tunasita kufanya ivyo tukihofia kuachwa pindi utakapo mwambia na tunasahau ukweli kuwa ni vyema zaidi mwenza wako kusikia kutoka kwako kuliko kuja kuligungua yeye mwenye kwani kama atakua amelifatilia na kulijua yeye mwenyewe itakuwia ngumu wewe kujieleza mbele yake hivyo maamuzi yake yanaweza kukuumiza na kukutesa. Kwahiyo kutokua muwazi kuusu maisha yako ya kweli, watoto ulio nao au ulie nae kabla yake, na mambo kama hayo yanaweza yaka sababisha mtu akaumia kwenye mapenzi
- Kutokutumia Moyo katika maamuzi ya mahusiano ya kimapenzi, unakuta mtu anamuacha mwenzi wake kwa kosa ambalo lingeweza kutatuliwa kwa njia nyingine na likaacha mahusiano yakiwa salama ila kutokana na kutumia mihemko ya hasira na chuki ndani yake anasahau mengine yote mazuri na matamu ya mpenzi wake na kuamua kumuacha alafu baada ya siku chache anaanza kujuta na kuumia na maamuzi yake ukuakirejea na kuyajutia maamuzi yake uku hakikili kua moyo wake bado unamuhitaji mpenzi wake huyo. hivyo matumizi ya moyo yana hitajika zaidi hususani katika kuamua maamuzi ya kipenzi.
- Kutokujihamini, unakuta mtu yupo kwenye mahusiano ila bado ajiamini na amini kama yeye ndio mmiliki wa mwenza wake au anashindwa kujiamini kwasababu mwenza wake anakua anamuhisi hisi vibaya. Haya yote mawili yanaleta maumivu na maangaiko katika mapenzi kwa maana hiyo basi bila shaka ili watu tusiumizwe na mapenzi ni muhimu kuamini kile ulichonacho na kuthamini kila unachofanyiwa na mwenza wako bila kuweka shaka katika kila kitu.
- Tabia ya kulimbikiza makosa ya mwenza wako na kuyatumia mala kwa mala kama ndo njia ya kujirinda pale unapomkosea, kama kuna tabia ambayo inanyima raha na kuumiza mahusiano mengi basi kulimbikiziana makosa ni tabia ambayo inatesa mioyo ya walio wengi. Mwanamke au mwanaume unamkosea leo unamuomba msamaha na yanaisha ila kila jambo linapotokea anakumbushia au wengine nao wanakukosea ukisema wanakukumbushia “mbona na wewe ulifanya hivi nami nlikusamehe”. Hii tabia pia inawafanya wengi washindwe kuendelea na mahusiano yao na wengine kubaki na madonda ndugu mioyoni mwao uku wakivumilia pendo kavu.
- Kufata maneno ya watu na kufananisha penzi lao la sasa na la zamani, niwape pole wale wote ambao maneno ya watu yalikua mwiba mkali katika mahusiano yao na wale ambao mwiba huo unaendelea kuchoma penzi lao ila ukweli nikua asilimia kubwa ya watu wanao umia na kuteseka na mapenzi ni wale ambao wapenzi wao wamejaribu kuwaacha watu wannje kuingilia mahusiano yao na wao wote kukosa msimamo juu ya hatma ya penzi lao pia wengine wanalia hususani ni wakiume unakuta mototo wakike anakomaa kuwa mbona zamani aukua hivo? Mbona sikuizi aufanyi hivi? Maswali ya hivo umuharibu zaidi akili na fikra za mwanaume kiasi kwamba anashindwa kujua ni vipi anaweza mfanyia mpenzi wake ili furaha ilejee na kuvifanya vile ambavyo alikua bora katika kuvifanya na hiyo hali umtesa na kuumiza na baada ya muda uchoka na magumu utokea hapo.
Hizo
ni baadhi tu ila yapo mengi sana hivyo ilikuweza kufanya mambo yawe safi katika
mahusiano yako kwenye blog hii tulishaposti njia za kuweza ku Imarisha penzi na
kulifanya lidumu ivyo fanya kulejea.
Na Charles N Matagi
No comments:
Post a Comment