NIMEKOSA NINI?
BARUA KWA MHARIRI
MPENDWA MHARIRI
Mimi ni mtafutaji kama watafutaji
wengine japo kuwa utafutaji wangu sio wa njia halali kwani mimi ni mwizi. Sio
kwamba napenda kuwa mwizi, la! hasha ila ni ugumu wa maisha ndio unao nifanya niwe mwizi ili tu kukidhi
mahitaji yangu.
- Nimejaribu kufanya kazi zote halali lakini nimekwama, yaani juhudi zangu zote zimegonga ukuta. Mwanzo,nilikuwa mchimbaji mdogo wa madini katika moja ya migodi hapa nchini kwetu, nilifanya kazi hiyo kwa muda sana kabla ya kuondolewa kwa kuambiwa kuwa hatuna vibali halali vya uchimbaji.
- Baada ya kutoka mgodini niliamua kuwa mvuvi, huko nako kulikuwa na changamoto zake kwani tuliondoa kwa kusema kwamba tunafanya uvuvi haramu.
- Kweli ng'ombe wa masikini hazai, niliamua kuchoma mkaa lakini huko pia kuna watu wa tulikutana na changamoto ya kupigwa faini kubwa sana ambayo inafahamika wazi kuwa hatuwezi kulipa kulingana na kipato chetu kidogo na kama si faini basi ni kifungo au vyote viwili kwa pamoja.
Ndugu zangu, nauliza nimekosa
nini!
- baada ya kuondolewa kwenye shughuli za kuchoma na kuuza mkaa nilamua kuwa machinga, bado ni karaha tu kwani kutwa kupambana na mgambo jiji wakitupiga na kuharibu bidhaa zetu ambazo mtaji wake ulipatikana kwa tabu sana kwa hoja ya kuwa eti tunafanya biashara kwenye maeneo yasiyo ruhusiwa
- kweli ni ngumu kutoboa kama hauna elimu yoyote katika dunia yetu yenye sayansi na teknolojia kubwa na huku viwanda mbalimbali vimefanya uwekezaji mkubwa wa mashine za kisasa ambazo zinafanya kazi zilizotakiwa kufanywa na watu zaidi ya kumi na hilo limenifanya kuwa si kitu kabisa na wizi kufanya ndo ajira yangu.
Ni maoni yangu kwamba ili kuweka
mambo sawa na wezi kupungua mtaani na kila pembe ya nchi yetu, kuna umuhimu
mkubwa kuanzia serikari ya kijiji, kata, wilaya mpaka serikari kuu kuhakikisha
vijana wote wanapata nafasi ya kushiriki kwa namna moja au nyingine katika
masuala ya ujenzi wa nchi iwe kimichezo, kiuchumi. Na kwa sisi wafanya biashara
wadogo wadogo waweke namna ya kutusaidi popote tunapokuwepo na biashara zetu
kupata utaratibu wa kuzifanya palepale bila kutuamisha hii itatusaidia kupata
nafasi pana ya kukuza uchumi wetu sisi na uchumi wa taifa hakika hapo sito iba
tena ntarudi kuuza dawa za mbu na vibiriti bila kum bugudhi mtu yoyote na kitu
chake nami ntatafuta vyangu la si hivyo mimi ntaiba mpaka pale mtakapo niadhibu kwa kipigo kikali na moto kwa kusema "yule mwizi wa muda mreefu leo zake 40 zimefika "kwani ndivyo mnavyo
amini kuwa kipigo na moto ndio njia ya kukomesha wizi.
na Denis M Nguno
(zawadi nono itatolewa kwa mtu ambae ataweza kuijibu hii barua kwa kutoa ushauri na njia thabiti za kuzuia wizi na kuwafanya wezi kupunguza wizi.
miongoni mwa zawadi hizo stori yako itakaa kwenye kurasa ya mbele ya blog hii kwa muda wa wiki
nzima
ukiandika tuma kwa watsap namba 0656109278 au barua pepe nelsoncharlesmatagi@gmail.com)
No comments:
Post a Comment