SIRI YA MAFANIKIO YAKO
"Uwekezaji bila kuanza na msingi wa
kujifunza ni mithili ya kuweka sukari kwenye sufuria tupu iliyowekwa katika moto
mkali".
Nikukaribishe ndugu mwana maarifa katika
makala haya ya jamvi la mafanikio, naamini maarifa haya yatakupa mwanga na
matumaini yaliyo jawa hekima kuelekea mafanikio.
ENDELEA KUSOMA>>>>>
KWANINI KIJANA ANAYE ISHI UCHUMI WA CHINI
KILA SIKU ANATESEKA KUTAFUTA KAZI?
Kufikia katika hatua ya maisha bora na yenye
matumaini halisi siyo kazi rahisi kama ilivyozoeleka sana lakini pia kwa maana nyingine
ni kazi rahisi pale tu mhusika ukifuata njia na mwongozo ulio bora wa wewe kuweza
kukufanya ufikie mafanikio makubwa.
- Katika kipindi cha miaka kadhaa ya hapo nyuma hasa miaka ya 1970, 1980 na hata katika miaka ya 1990, watu ambao walipata nafasi ya kwenda shule na wakabahatika kufika hadi hatua ya kupata elimu ya juu yaani chuo kikuu walijawa na matumaini makubwa mno ya kuhitimu masomo yao kisha kujipatia ajira walizosomea"Taaluma"chuoni kwa kipindi chote cha maisha ya elimu yao.
- Katika kuliangazia hili siyo kweli kwamba hawa wahitimu walikuwa ni wabobezi sana hali inayo watofautisha na wahitimu wa hivi leo, la!! hasha tatizo ni hali ya uhitaji na upatikanaji wa nafasi za ajira ulikuwa ni mkubwa na wasomi walikuwa ni wachache. Sasa hali hiyo ya kipindi cha nyuma huwezi kuilinganisha na miaka ya 2000 hasa mwanzoni mwa karne mpya ya 21 ambapo katika kipindi hiki maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia yalichukua hatua kubwa zaidi licha yakuwa hapo nyuma yalitawala kwa kiasi chake. Ufinyu wa nafasi mbalimbali za upatikanaji wa huduma kama vile elimu ambayo milango ilifunguliwa kwa upana hasa katika bara la Afrika na nchi zilizoko kusini mwa jangwa la sahara baada ya uhuru, kutokana na kuwepo kwa nafasi chache na huduma ambazo hazikukidhi mahitaji katika nyanja mbalimbali hasa kwenye upande wa elimu, upungufu wa shule,hospitali na barabara na hata vyuo vikuu ilipelekea serikali na vyombo mbalimbali kuhitaji zaidi wafanyakazi kukamilisha malengo mbalimbali ya vyombo hivyo au jamii kwa ujumla hivyo uwezi linganisha na hivi sasa.
- Katika kipindi cha miaka ya 2000, maendeleo na fursa mbalimbali zikafunguka zinazompa kijana upeo mpana wa kufikilia ni ipi njia sahihi na wezeshi ya yeye kuchukua ilikufanya kijana kuzidi kuiishi ndoto zake hatimaye kuja kuyafikia mafanikio mapana na bora hapo mbeleni. mbali na ufinyu wa ajira lakini huu ni wakati mwafaka na sahihi kwa kijana kuchukua kulingana na fursa zinazo mzunguka kulingana na mazingira yanayo mzunguka.
- Hivyo, kutokana na hali na mfumo uliozoeleka na unaotumika kwa baadhi yetu sisi vijana ambao tumebahatika kupata mtaji mkubwa usiofilisika kirahisi tuliopewa kwa mchango mkubwa wa wazazi/walezi na serikali yetu ya Tanzania yaani "Elimu" bado tupo tu na hatuchukui hatua yoyote ya kujikwamua kutoka kwenye hali ambayo sio halisia kwetu kulingana na elimu na ujuzi tulionao vichwani mwetu hali ya umasikini na wengine tukisubili ni lini tutajipatia ajira kutoka kwenye taasisi/mashirika mbalimbali kitu ambacho naamini sio sawa kusubiri wakati kuna mengi ya kufanya ilitutoboe tobo la mafanikio yavujie upande wetu.
- Lakini wakati wewe ukiwa unasubili pengine kutafuta kazi angali ya kuwa unao mtaji wa kutosha yaani elimu, yupo kijana mwenzio aliyetazama fursa na anaendelea kuwaza na kuchukua hatua za mapema zaidi kwa kutumia ubunifu alioupata kutoka shule na chuo kuanzisha mradi utakaomfanya kubadili historia yake ya maisha yake na familia yake, hatimaye jamii na nchi yake kwa ujumla hivyo ni muda wetu kupiga kazi.
- Kwa kipindi hiki tulichopo sasa dunia imekuwa kijiji unaweza kujifunza mambo kwa upana sana, mambo ambayo yanahusu maendeleo yaani ni kwa jinsi gani na hatua zipi uchukue kufikia mafanikio, kwani teknolojia tukiitumia ipasavyo kwa ufanisi na ufasaha kama nchi zilizoendelea wanavyofanya hakika suala la utegemezi wa kutafuta ajira litakuwa limepungua kwa kiasi kikubwa au kuhisha kabisa hasa kwa nchi zetu zinazo endelea hivyo amna mwingine zaidi yako wewe na mimi kuhakikisha tunafanya kweli kukamilisha au kuandika historia mpya za maeneo yetu tunayotoka.
- Sasa basi, ili kukaribia na hata kuifikia hatua hiyo vijana tunapoingia shule na vyuo vikuu tuhakikishe tunayaache mawazo tuliyo aminishwa pindi tunaanza masomo yetu tokea darasa la awali, shule ya msingi na sekondari ambayo wazazi na walezi wetu walisema maneno kama...."mwanangu jitahidi kusoma kwa bidii sana ufaulu vizuri ufike hadi chuo kikuu na baada ya kuhitimu UTAPATA AJIRA na maisha yako yatakuwa bora". Hama kwa hakika vijana tunapashwa kutambua na kubadili fikra zetu tulizoaminishwa ili tuweze kufanya yale wanayoyahisi ni magumu kufanyika katika kwanjia ya kujiajiri. Au tutumie kuaminishwa huko kuwe chanzo kwetu sisi kupiga hatua thabiti za kuyafikia malengo yetu.
VIJANA MBONA MAMBO YENTE.
👍👍👍👍
Mwandishi ni Boniphace Gogo
Mawasiliano: +255744016068/0784550330
No comments:
Post a Comment