BARUA KWA MHARIRI
MWALIMU
Na Charles N Charles
Mpendwa mhariri,
Nimeona leo nikuandikie
labda huenda na mimi nitasikika na kwa utambulisho tu mimi ni yule mwalimu mkali, mkorofi na muda
mwingine wanafunzi nasikia wananiita diktekta. Na sikatai, ukweli ni kwamba mara
zote nimekuwa karibu na kiboko changu cha kuwanyoosha wale wanafunzi ambao ni
changamoto katika ufanisi wa kazi zetu, sio kwa maagizo yaliyomo kwenye biblia
(Mithali. 23: 13) kwamba “usimnyime mtoto wako mapigo’’ la hasha! ila nina mengi
ya kumtumia rafiki huyu fimbo kama njia yakuwanyoosha na kuwafanya wanafunzi
wangu waweze kuwa watu bora hapo mbeleni na nikazie kwa kuwakumbusha tuu kuwa nitawachapa.
- Ukiachana na nyumbani, shule ndo mahala pekee kwa watoto na wanafunzi kujifunza na si kwinginepo, sasa ni vipi nitamudu idadi kubwa ya wanafunzi wanaonikabili katika zamu yangu? Hali ya kuwa walimu tupo wachache tunafichwa na idadi kubwa ya wanafunzi. Acha nilalame bila mwisho nawezaje chagua tui la nazi ni lipi na maziwa ni yapi katika muda mdogo tu wa asubuhi na kulinganisha na wingi wao eti ni vipi nimjali mtoka mbali aliechelewa ili hali yakuwa watokambali wenzake wamewahi? Hakika sina sababu ya kumuacha nitamchapa tu.
- Mazingira magumu ya nyumbani na michezo, huku kuchati kunamkabiri analala usiku ukiwa umeenda sana, anakuja darasani kulala kwenye kipindi changu cha asubuhi na hapo pia nisimchape? Sasa namfundisha nani wakati yeye amelala! Siwezi lamba asali kwa nncha ya kisu hakika nitamchapa
- Natoa mazoezi kila nikitoka darasani, naelezea wanasema wameelewa na maswali wanauliza majibu nawapatia. Je, ni nini sijawafanyia? Madaftari yao nukuu nimewajazia na samari nimewapatia bado nawauliza nini sijawafanyia? Kengele ikigongwa wote nyumbani wanakimbilia masomo ya ziada najitoa kuwafundisha ila wao wanapuuzia na majina mabaya wananipatia. Bado wakifeli wanataka niwashangilie, kwa jitihada zangu zilizo potea? huyo sio mimi! acha wafeli viboko wataogelea.
- Nawapa pole sana Abdalah, Zuhura na Pendo na makundi yao, hivi ni kweli hawajawaona Asha, John na Mwamini ukaribu wao na walimu ulivyo mea? mnaishi mazingira hatarishi na wanaowataka ni wakubwa kwenu mnahitaji ushauri na ushirikiano na walimu kukomesha jambo hilo, sasa kwanini muogope katika haki yenu wakati nikiwachapa nawachapa kwa makosa yenu? Kweli nitazidi shindwa kuwaelewa kama hawato hudhuria katika darasa langu kwa kweli nitawachapa
- Kwa saikolojia ndogo tu nawaona ni watu wanaoshindwa na kuhangaika. Hivyo acheni hizo sababu na anzeni kutimiza wajibu wenu huku mkipunguza mambo yasiyo na msingi, someni mpaka mwisho na msikubali kuwa watu wa kutafuta visingizio, kweli someni someni mpaka mwisho, pambaneni bila kuchoka kwani hata Suzan pia nae ni mwanafunzi mbona yeye hachapwi na adhabu hapati! Basi kumbe njia pekee ya kubadilisha mfumo ni nyinyi kuanza kubadilika ili mfumo ubadilike kufuata mabadiliko yenu.
Kwa maoni yangu, ili
mimi na wanafunzi wangu twende sawa ni lazima kila mmoja wetu ahakikishe
anatimiza wajibu wake na kufata utaratibu uliowekwa shuleni, kwa upande wao wasome
kwa bidii wafanye kazi zote za shule watulie madarasani na mimi nitawafundisha
kwa weledi, pia kuwashauri wanapokwama. Hiyo itakua ni njia pekee ya mimi na
wao kwenda sambamba na kuwalinda kikamilifu. Ila kwa hapa mwanzo mimi nitashika
kiboko changu pamo
ja na uwajibikaji wangu mpaka watakapobadilika pia na wao wajitahidi
kujali majukumu yao yanayo wahusu wao kama wanafunzi na wayatimize ipasavyo.
(picha zote mtandaoni)
No comments:
Post a Comment