LINZA WA MAMA
Simulizi sehemu ya kwanza
- Msimulizi
: linza ni binti aliefanikiwa kumaliza elimu yake ya kidato cha sita na kupata
nafasi ya kuendelea na elimu ya juu nchini Tanzania. Akiwa ni
binti pekee katika familia yake, kama ilivyo desturi na mila za watu wa Afrika wakati Linza anaenda
chuoni wazazi walipata mda wa kumkanya na kumsii afuate mienendo
iliyo bora akiwa chuoni hama kwa hakika afuate kilicho mpeleka.
Mama
Linza : Linza mama
Linza :
abee mama
Mama
Linza : Linza mwanangu tunakuomba
ukasome, ukasome utatutoa katika umaskini huu tulio nao mwanangu, nakuomba ujifunze uko
chuoni mwanangu usijetutia Aibu wazazi wako.
Linza :
ndio mama jamani ntasoma kwa bidii ata usiwaze mama angu kweli sito kuangusha.
Baba
Linza : ukasome kweli ooho!! Mtaani maisha ndo kama unavyo yaona kasome linza.
(mama
anadakia )
Mama Linza : eeeehe!! Linza unaona mzee wako kashaanza
hapo kuongea anaweza kuongea mpaka mapambazuko nenda kajiandae kesho
safari mwanangu, na usisahau na kile kitenge pale juu ya kabati mwanangu...
Linza : (kwa kujivuta ananyanyuka na kwenda na kwenda
chumbani kujiandaa akiwaacha baba na mama yake wakizungumza
hili na hile)
- Msimulizi : ni siku ya tatu sasa tangu Linza aingie
chuoni , na akiwa darasani hapo anakutana
na Zubeda na Avijawa na kuanza kujenga mazoea, huku
Zubeda na Avijawa hawa wote mbali na
chuo pia walikuwa
ni wadada wa mjini wakihuzuria na kujichanganya pande pande zote za
starehe bila kujari. Jambo ilo liliwafanya wajuane na
Juma ambae pia alikua ni mzee wa kuluka kwanja.
Juma : ni adje wadada!! Naona mupo mnajaribu kutazama
michongo
Zubeba : michongo wapi Juma..!!? si tupo tu hapa
tunajarbu fikiria wapi pa kwenda si unajua wikiendi hii...
Avijawa : tena bora nimekuona Juma hivi ulisema unakomplimentari za klubu gani kwenye
group..?
Juma : (uku akicheka) Avijawa bwana zile ni za fifte
five ni leo usiku kuna kanga moko vipi mnataka kwenda..?
Zubeda na Avijawa : (wakajibu kwa pamoja) sio la
kuuliza ilo Juma, tupe tupe tukajiandae sie(wanacheka cheko ya kimbea na
kugonga)
Juma : (anaeka koo sawa na kuongea) afu nyie vipi
mbona mnaongea nyie tu, mbona mwenzenu yuko tuli.
Linza : (uku akijitanua kifua) amna tu nilikua
nasubiri wamalize si unawaona walivyo wapana hao
(wote wanacheka)
Juma : okey
kwahiyo Avi si utakuja na huyu mrembo klubu au unasemaje mrembo?
(juma anamuambia
Avijawa huku
akimuangalia Linza nakuuliza kaswali kauchokozi).
- Msimulizi : mambo hayo..!! Linza, Juma, Avijawa pamoja
na Zubeda walienda klubu kuburudika na kushuhudia usiku wa kanga moko,
na kama unavyojua mambo ya klubu kila mtu alichukuliwa na mtu wake na kufanya Linza na Juma kubaki
wenyewe wakicheza muziki na kuonyeshana uhodari kwa kadri walivyoweza kiasi kwamba walipata kupeana
raha. Nakila mmoja alikili kuwa mwenzie ni kiboko katika sekta ya
kukata ngoma, baada ya muziki Juma na Linza walielekea geto kwa Juma
ilikumalizia usiku huo.
club
- Msimulizi : ikiwa ni saa tatu asubuhi Linza
anashtushwa na mlio ulio ambatana na
mtetemo wa simu yake huku akiwa na wenge la usingizi anaangalia ni nani
anapiga gafla anashtuka.
Juma : mbona umeshtuka ivo ni nani..?
Linza : ni mama tafadhari usiongee..!
(Linza anapokea simu na kuuanza kuzungumza na mama
yake)
Mama Linza : hallo.!! Linza mwanangu mbona huko kimya
sana
Linza : ni ubize tu wa chuo mama ila vipi nyinyi
wazima huko?
Mama Linza : sisi wazima mwanangu hofu yetu kwako vipi
masomo
Linza : safi tu mama yaani nimechoka hapa jana
nlichelewa kweli kulala tulikua na diskasheni mpaka saa nne nkapitiliza kusoma
mpaka saa sita kwakweli nimechoka mama.
Mama Linza :pole mwanangu, basi acha nkuache upumzike
tutaongea baadae mwanangu masomo mema.
Linza : asante mama
(anakata simu na kushusha pumzi kwa nguvu na kumtazama
Juma aliekua amekaa huku akifatilia mazungumzo hayo na wote wana cheka cheko
ndogo)
- Msimulizi : mh!! Mtazamo wa mama Linza juu ya mtoto
wake ni tofauti kabisa na ukweli kuusu linza ambae sisi tunajua wazi ya kuwa
kamaliza usiku mzma akiwa na na Juma. Nakutokana na kufurahishana wakawa awana
namna zaidi ya kuanzisha penzi lao jipya.
Juma : mama anasemaje my
Linza : mh! Utawaweza hawa wazee awana la kusema
usijari wangu ni yaleyale
Juma : okey mamaa sawa, afu Linza sasa tunafanyaje
mama kwa maana we mtoto ni moto
Linza : (kwa sauti yenye kaaibu kwa mbali)mi sina la
kusema Juma ni wewe tu.(anaangalia chini kwa aibu)
Juma : sa unaonaje uje tukae wote hapa (juma
anachombeza)
Linza : Juma jamani mbona mapema hivo mi naogopa
Juma : (kwa cheko ya mbali na kuongea kwa mkazo)
usiogope mamie kuwa huru mda wowote tu karibu hapa sas ni kwako
Linza : sawa J asante ntajaribu kufanya hivo taratibu.
JE Linza atakubari kuja kuishi na Juma? na nini kitafuata? itaendelea
usije kukosa kisa hiki
- (tutakua tunatuma hadithi kila baada ya siku mbili )
No comments:
Post a Comment