Na Denis M Nguno
Nakumbuka nilipokuwa mtoto, kwangu mapenzi nilijua ni something very Yuumy
but no sivyo hivyo.
Now nimekua mtu mzima I even dont need
to hear neno NAKUPENDA sababu moyo wangu upo kwenye life supporting machine
kwasababu tu ya mapenzi.
Kwani hapo mwanzo nilipata mpenzi ambae
alikuwa anaitwa Anitha ambaye I really loved her and treated her like a Queen
but guess what I was a fool amongest fools nilikua najitahidi kutunza kumbe
wenzangu wanalamba tu ikafika muda
nkagundua lakini ilikua too late nililia sanaa. Na nakili ilikua ngumu
kwangu kumsahau lakini mwisho wa siku nilimsahau na kuendelea na maisha yangu
ya kawaida.
- Baada ya muda nikiwa sina hili wala lile nikajikuta kwenye penzi zito sana na mdada mrembo Jennifer kwangu Jennifer nilimuona kama malaika kutoka mbinguni kwa ajili yangu Hahahahahahaaahaa, Mpenzi huyu tulifikia hatua mpaka ya kuwekana mitandaoni yaani alikua kazipamba all my social media kwa kusifu na kuliombea penzi letu kwakweli I saw her like my breath actually she was one.kama kawaida ya mapenzi moto sikuwa naweza kupitisha nusu saa bila kumtxt "Hellow my love za muda nishakumiss mwenzako" na ananijibu "Ooh babe nimekumiss pia sana sanaaa me niko poa how bout you???" basi akijibu hivyo mimi roho yangu kwatuu nilikua natembea navimba kana kwamba nina majipu makwapani. I wished to tell the whole world how much I loved my little angel. Lakini Jennifer wangu nilidumu nae kwa mwaka mmoja tu na hapo ngendembwe zikaanza mara hajibu txt ,mara yuko busy, niliumia sana but kila nilipokua nikimwambia alinambia ni kubanwa na kazi kidogo tu but everything will go back to normal. One day I woke up na nikakuta txt yake eti Denilson siwezi tena kuwa na wewe nimepata mwanaume bora kuliko wewe please dont even txt me maisha mema.Nilijua ni utani kumbe ilikua kweli daaah ...Nilijaribu kupigania penzi langu kwake lakini nilikwama nilikuwa kama vile nasukuma ukuta ambao kamwe hauwezi sogea.So nikajisemea moyoni kwamba sasa mimi Mapenzi baaaasi sitaki tenaa.
- Pigo hili la pili lilinipa kidonda juu ya kovu lile la mwanzo. Na hapo pombe ilikuwa ni rafiki yangu wa karibu sana sababu binadamu wote niliwaona kama wote ni wanafiki na sikutaka kuwa karibu nao kabisa, Baada ya hiyo breakup nilikaa muda mrefu sana bila ya kuwa na mpenzi but kwa sababu moyo umeumbiwa kupenda then I felt like I needed someone ndo hapo nikaamua kutafuta mwanamke ambae nilitamani sana awe mwanamke wa maisha yangu, baada ya sakasaka ya muda nilimpata Gift. Kabla ya Gift na mimi kuwa wapenzi nilijaribu kumchunguza anapenda nini na nini hapendi na nilifanikiwa kujua nini anapenda na nini hapendi kama wafanyavyo wanaume wote wenye nia ya dhati kwa mwanamke mmoja na wapekee kwenye maisha yake.
- Siku moja I decided to invite her to my place na alikuja kwa muda tuliokubaliana, nilijipanga kumwambia what I felt for her but haikua rahisi kwake kunikubalia kwa kusema kwa muda huo hakua tayari kuwa kwenye mahusiano so she asked for a time anifikirie na nilikubaliana nae, after a week na siku kadhaa alinikubalia, kwa kweli nilifurahi sana kuskia hivyo kama mtoto anapokua kaletewa nguo mpya kwaajili ya sikukuu.
- Na pia mapenzi yetu yalianza kwa moto sana, sikutaka kupoteza muda I introduced her to my squad kwanza. Na pia kwenye siku za mwanzo I told her everything about my past na nilivyoumizwa na ma ex wangu. Kwakweli alionekana kunionea huruma sana na She promised not to leave my side na aliniambia kwamba nimempata yeye mwenye penzi la kweli kwangu kamwe hatoniumiza.
- Mimi na Gift tulipendana sana na tulithubutu kuitana Mume na Mke ,hahahah yaani ananiita Mume wakati hata kwao sipajui wala kwetu hajawai fika, huu ni pia ulipata kuwa upumbavu wa grade A naweza sema. Mimi na Gift tulidumu kwa miaka 2 kabla ya jini kisirani kuingia kwenye utamu wa penzi letu. Siku moja one of my best friend ambaye we called each other brother, aliniomba namba ya shemeji yake na sikuona ubaya nikampa namba na ndo hapoo shida ikaanza. Sikujua rafiki yangu alikua na lengo gani na Gift(shemeji yake), kumbe he was dying to be with her, (Zacharia) rafiki yangu alifanikiwa kumrubuni Gift so wakaanzisha mahusiano yao kwa siri.
- Mungu sio Athumani wala Abdallah Ismail siku moja niliwafumania kwa rafiki yangu ( Zacharia) my brother Hhahah daah sikuamini kama wangeweza kunifanyia hivyo, Niliondoka kwa hasira na kurudi kwangu, After an hour Gift alinipigia simu wala sikutaka kupokea simu yake, alituma messages pia sikujibu. Aliamua kuja kwangu eti kuniomba msamaha, eti yaani anaomba msamaha kwa jambo ambalo aliamua kufanya akijua fika kwamba sio sawa. Nilimfukuza na kumwambia siwezi kumsamehe, sikutaka kumsamehe kwa kinafiki though it wasn't easy. So I lost a woman whom I loved so much and I also lost a best friend a brother.
From that day sikutaka kusikia story
about Mapenzi. Kwasababu nachukia mapenzi, yaani nachukia mapenzi for
really nachukia mapenzi.
"Mapenzi" what a despicable thing.
Ni historia ya
kweli
Majina sio halisi
No comments:
Post a Comment