JE WAJUA KWAMBA FARU WA AFRIKA AWANA MENO YA MBELE?
FARU
kifaru akiwa hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, picha na mtandaon |
Kisayansi - DICEROUS
BICORNIS (Black rhino)
- CERATORETHIUM SIMUM (White
rhino)
Faru ni miongoni mwa
wanyama ambao ni Big five kwa Afrika, wengine wakiwa ni chui, simba, mbogo na
tembo. Kuna aina tano za faru duniani; faru Javan, faru Indian, faru Sumatran,
White faru na Black faru. Faru Javan na
faru Indian hawa ni jamii ya faru ambao wana pembe moja usoni mwao na Africa tuna aina mbili za faru ambazo ni faru
mweupe(White rhino) na faru mwesi(Black rhino), aina tatu zingine zinapatikana
bara Asia. Tanzania sisi tunayo aina
moja tu ambayo ni Black rhino, ingawa tuna white rhino ambao wanapatikana
Mkomazi National Park ambao ni” introduced spicies” waliochukuliwa kutoka
Afrika ya kusini.
- Faru pia ni miongoni mwa wanyama ambao wapo hatarini kutoweka duniani kutokana na kuwindwa sana na majangiri sababu pembe zao zina thamani kubwa Barani Asia kwani pembe hizi hutumika kutengeneza dagger”visu vikali sana” pamoja na dawa za kuongeza hamu ya tendo yaani (VIAGRA).
- Faru hasa vijana huishi mmoja mmoja yaani “solitary” pia dume na jike hukutana wakati wakujamiiana pekee ambapo kama itatokea faru jike anapata ujauzito basi itamchukua miezi kumi na nane (18) mpaka kuzaa na kiuhakika faru anazaa mtoto mmoja tu kuzaa mapacha ni mala chache sana. Faru hutumia zaidi ya dakika arobaini(40) wakati wakujamiiana na tendo hili hutokea baada ya faru dume kuhisi harufu maalum kutoka kwa jike, harufu hyo hutolewa na faru jike wakati wakuzaliana tu.
- Katika suala la maisha faru anapendelea zaidi kuishi kwenye maeneo ya tambalale na vichakavichaka huku kila faru mmoja akiwa anamiliki eneo lake na wanyama wa aina hii wanaoishi kimipaka kitaalamu tunawaita Territorial, na kama faru ataishi sehemu salama faru anaishi kuanzia mwaka mmoja mpaka therathini(30) na wengne ufika mpaka hamsini(50). Na katika kuishi baada ya mama faru kuzaa katoto kake ukaa nacho mpaka kanapotimiza miaka miwili mpaka mnne ndipo umfukuza akaanze kujitegemea uku mtoto wa faru baada ya kuzaliwa anaanza kula nyasi anapo timiza wiki moja tu.
- Licha ya mwili mkubwa wa mnyama faru ila ni miongoni mwa wanyama wanao ona vizuri sana mchana uku usiku kwao kiwa ni mgumu kuona vizuri, na tofauti na jamii zingine za faru, faru wa Afrika awana meno sehemu ya mbele ya midomo yao,licha ya kuishi kwa kujitenga na kuishi kwenye imaya yake yenye 12 kilomita za miraba kipindi cha masika na kipindi cha kiangazi upanua imaya yake mpaka kufikia 20 kilomita za mraba faru anatumia vizuri pembe zake kumsaidia kupambana na adui zake wanaotaka kumzuru na kulinda mipaka yake. Ukiachana na mwili mkubwa wa faru ila anauwezo wa kukimbia kilimita 40 kwa saa.
faru akiwa mbugani picha na Jungle Empire Africa |
1 comment:
like it
Post a Comment