WE MUHESHIMU TU! ATA KAMA UNAJUA HALI YAKE…………..
Katika maisha ya
mwanadamu ya kila siku tunasahau kitu kimoja ambacho ni muhimu sana hii
yote wenda ikawa inatokana na kulidhika na hali uliyokuwa nayo kwamba uko juu
au ni una mazingira mazuri. Leo napenda
kuja na wazo kama hili kwamba katika maisha siku zote usipende kudharau kwanza
mawazo yako lakini pia usipende kumdharau mtu yeyote. Vijana tulio wengi HASA
kabisa wasomi wanapenda sana kudharau wasio kuwa wasomi na kuwaona kuwa
wamepotea kutokana na hatua waliyo kuwa nayo. Hadi inafika hatua basi wale
wasio kuwa wasomi wanajihisi wametenda dhambi isiyosameheka .Ewe wewe ndugu
yangu msomi embu fikiria hatua ulizo pitia mpaka kufikia hatua hiyo umepitia mangapi wangapi wamekushika mkono
ulipo dondoka na kukuambia bado safari inaendea unashangaa wengi kati yao
hawakufikia katika hatua hiyo uliyokuwa nayo wewe japo kuwa walikunyanyua pindi
ulipodondoka hii yote kukutakia mema wewe ili ufikie hatua Fulani basi wewe
kisa tu umeenda chuoni unahisi umefuzu kwenye milango ya PEPO haya ni maisha tu
na bado safari inaendelea .Nasikitishwa sana na vijana ambao wamefika katika
elimu ya juu basi wanaporudi wanapoona wenzao wako nyumbani huwadharau na
kuhisi hao wamepotea kumbe hata hao walihitaji kuwa nafasi hiyo ambayo wewe upo
kikubwa mshukuru MUNGU kwa kukuweka katika daraja hilo kwani sio kwa ujanja
wako.Unarudi nyumbani baada ya kutoka chuo basi hata salamu tu inakuwa shida
eti ukidai uko bize asee. Muheshimu kila
mtu usiangalie ana umuhimu gani katika maisha yako au ananafasi gani katika
maisha yako .Kwani unapokuwa mnyenyekevu kwa mtu unapungukiwa na nini elimu
yako ndo ikafanye udharau watu ???
NA FADHILI TAJI
No comments:
Post a Comment