KONA YA MWANAMAARIFA
Tunajifunza mambo mengi katika dunia na katika maisha lakini
kuna mambo tunatakiwa kuishi nayo.
Kamwe usiache
kujifunza kwa namna yeyote ile.
~Tumia maarifa uliyonayo kupata unachotaka ila usiache
kujifunza maarifa mapya.
Kuna siku nilikuwa nafikiria kwamba ya mkini watu waliofariki
miaka ya nyuma ikiwa watakuja duniani tena wanaweza wakawa wanashanga shangaa
tu jinsi dunia ilivyobadilika na watu wenyewe pia.Maisha ya sasa yameambatana
Na mabadiliko mbalimbali kwenye nyanja karibuni zote.
Hivyo basi karibu kila siku mtu atahitaji kuji'tafakali' ili
aende sawa Na mabadiliko hayo ya sayansi na techonolojia. Wanasema mabadiliko
ni lazima yatokee na ubaya Wa mabadiliko ni kwamba usipokuwa tayari kubadilika
kwa hiyari yako,yatakulazimisha yenyewe kubadilika( utabadilika kwa lazima)
Mara nyingi napenda kusema;
"USIPOTAKA
KUJIFUNZA HAKUNA ATAKAYE KUSAIDIA KUJIFUNZA,NA UKITAKA KUJIFUNZA HAKUNA
ATAJAYEWEZA KUKUZUIA". Kila kitu kipo ndani ya uwezo na maamuzi yako
mwenyewe.
Usiache kujifunza kwa sababu maisha hayatachoka
kukufundisha.Inawezekena kiwango chako cha elimu ni shahada au stashahada
pengine ni masters au PhD usiache kujifunza pia.
Kumbuka kila siku Duniani kunatokea mabadiliko mapya
unayohitaji kuyajua ili kuboresha maisha yako.
Ndugu mtaani kunahitaji
maarifa zaidi ya hayo usiache kujifunza zaidi kwa kiburi cha Elimu yako na
cheti ulichonacho.
Imeandaliwa
na Pascal Mtani
No comments:
Post a Comment