KAMA UMEJIPAKA UPUPU, WATU WOTE WANAKUKIMBIA
Charles N Matagi
aliwazalo mjinga,
ndio litakalo mtokea
uliishi kwa ujanja,
na maisha ukayazoea
leo unaliona janga,
na nyumbani unaelekea
hukukumbuka kujenga, hukujua
yatayotokea.
mwisho wako kunywa supu,
mihogo na magimbi utajisevia
mikononi sasa mtupu,
kwenye umaskini umerejea
kama umejipaka upupu,
watu wote wanakukimbia
hapo kwako patupu, hauna
wakukusaidia.
hakika unayo nafasi,
tena bila wasi
unaweza lima
mananasi, kilimo akito kuasi
cha msingi uwe na
kasi, hakuna mwenye mkosi
simama ungana nasi,
utashika moja nafasi.
umejua dunia ni
mwalimu, acha kujilaumu
nafasi hii adhimu,
umeipata weka utimamu
achana na uchakalamu,
andaa yako kalamu
tena kula kwa
nidhamu, na azina itadumu.
…………tumia kwa nidhamu
kuchuma umeuona ugumu……….
No comments:
Post a Comment