MAMBO YANAYOWEZA KUATHIRI UKUAJI WA MTOTO
Na Charles N Charles
Himezoeleka kwa wazazi na walezi wengi hususani wazazi wa nchi za kiafrika kwamba kutumia maneno yakukataza, ukali na lugha ngumu kwa watoto wetundio njia ya kumjenga mtoto mwenye heshima, adabu na mafanikio hapo mbeleni. kitu ambacho kinapingana na ukweli kwamba kwa kuwafanyia hinyo watoto wetu badala ya kuwajenga kama tunanyo waza tuwahalibu na kuwapa wakati mgumu watoto hao katika hatua zao za ukuhaji. Leo tutaongea baadhi ya mambo na maneno yanayo vunja na kuharibu ukuaji wa ndani na nnje wa mtoto na kumfanya mtoto ashindwe kufanya mambo mbalimbali ya kimaendeleo kikamilifu kulingana kasi ya maendeleo ya sayansi na teknologia inavyokwenda.
- Matumizi ya neno (usi), kwa mfano usiguse, usichezee, usilalie,usifanye, usijaribu nakadharika. Familia nyingi na watoto wengi wanakosa hali ya uthubutu na kujiamini tu ni kwasababu amekua katika mazingira ambayo kila kitu anachojaribu kukifanya anakutana na neno (usi), na niwazi kwamba kujua na kuelewa mambo kupo katika kujaribu. kadri unavyo mzuia mtoto kujaribu hili na lile wakati anakua hiyo hinamfanya hapoteze uwezo wake wakujiamini na kutaka kujua mambo pia uthubutu unakoma ndani yake hali inayopelekea mtoto kuwa tegemezi na kushindwa atakujiajiri au kuthubutu kufanya chochote mpaka mzazi au mlezi umuamuru kufanya hali ambayo inahathili moja kwa moja uwezo wake wa kufanya maamuzi na kuwa goigoi.
- Wazazi kutumia maneno ya kukatisha tamaa kwa mfano baada ya majibu ya mitihani kutoka,utasikia mzazi anasema" yani nlijua tu utafeli amna kitu hapa nlipoteza hela zangu bulee”. Ukianzangalia biblia ukasoma Mathayo Mtakatifu 14: 24 – 31 utaona ni jinsi gani Bwana yesu aliruhusu mtumishi wake Petro kujaribu kutembea juu ya maji na alipo shindwa alimsaidia na kumwambia shaka ni tatizo lililomfanya akashindwakuimilikutembea juu ya maji akiwa na maana halekebishe na kutoa shaka yake na siku nyingine afanikishe na kuishinda shaka iliyondani yake. kwamaandiko hayo basi ni vyema mzazi tukatumia lugha sahihi ya kutia moyo kwa watoto pale wanapojaribu nakushindwa kwakuweka wazi tatizo ilikuakikisha watoto wetu wanapata ujasiri wa kusonga mbele na kutimiza malengo yao kikamilifu.
- Mila na desturi kandamizi, bado kunabaadhi ya mila na desturi ambazo zimeendelea kushikiliwa na baadhi ya wazazi au walezi juu ya makuzi ya mtoto ambazo zinamfanya mtoto kujiona yeye ni wa chini na sio wa kuweza kufanikisha mambo au jambo lolote, kwa mfanowatu wa mikoa ya kanda ya ziwa wao wanaamini katika kumsomesha mtoto wa kiume na kumtenga na kazi za nyumbani pia kumpa majukumu ya kuibeba familia kama kiongozi huku hikimpa nafasi fenyu sana mtoto wa kike katika Nyanja ya elimu na kukuza uchumi wakiamini kuwa mtoto wakike sio mali ya nyumba hiyo yeye ni kwaajiri ya kuolewa na kupambana na kazi za nyumbani.hali hii inapelekea watoto wengi wakike kushindwa kujisimamia na kujiona wao ni duni mbele ya mwanaume au jamii na ivyo inapelekea kuvunja na uharibifu wa malengo na jitihada za kutaka kufanikiwa katika maisha yake na kukuza utegemezi.
- migogoro ya wazazi pia huathiri ukuaji wa mtoto kwan migogoro ujenga hofu ndani ya mtoto na kufanya ashindwe kufanya vizuri ata kile alichokua anakimudu vizuri hapo mwanzo
Jambo lingine nikutokuwaamini watoto wetu katika kilajambo analolifanya, kwakawaida kila mtu duniani anapenda kuaminiwa inapotokea unafanya kitu angali ya kuwa unajua wazi watu awakuamini na wanaona utashindwa inamvunja mtu moyo wakujiamini katika utendaji wa jambo ilo hali hii pia inatokea sawa sawa kwa mtot asipo aminiwa basi hali hiyo inavunja imani yake na kujiamini kuwa anaweza na kujikuta anakuwa ni mtu wa tegemea zaidi msaada kutoka kwa wazazi au walezi wake.
(chanzo cha picha ni mtandao)
No comments:
Post a Comment