KWANINI TUSIAMINI KWA KILE TUNACHOKIAMINI KUWA KITATUFIKISHA KWENYE MAFANIKIO?
Na
Charles N Matagi
karibu tena ndugu msomaji na
mfatiliaji wa mada zangu leo naongea na kijana mwenzangu ambae anataka kufika
sehemu ya mbali kimafanikio ambayo anaiwaza na anaitamania kufika ila hajui ni
kwa namna gani anaweza akafika pasipo kuwa na shaka loloote. Nakuja na hatua tano za kutoboa
na kufikia malengo.
- Angalia umbali unaotaka kwenda, kwanza kabisa kijana ni lazima ujue ni wapi unahitaji kufika kimafanikio kwani kwa kujua hilo litakusaidia kujua ni aina gani ya watu inabidi uwe nao, ni mambo gani ya msingi inabidi uyafanye kuhakikisha unafika unapokwenda salama. Mbali na hilo pia kwa kujua umbali unao kwenda utakusaidia juu ya suala zima la kupanga na kugawa muda wako ili kufanikisha ipasavyo safari yako inakua njema na ya mafanikio.
- Kujua aina ya wasafiri ambao unasafiri nao katika safari moja, je! Wote mnamalengo sawa na wote mnania ya kufika mnako taka kwenda? Kwani katika safari ya mafanikio kila mtu ananjia na namna ambayo anaona yeye ni sahihi kwake kutumia kufikia mafanikio aliyo jiwekea hivyo lazima ujue ni aina gani ya marafiki au washirika ulio nao katika kukamilisha safari yako ya mafanikio.
- Futa historia yako ya nyuma, hili ni jambo kubwa sana ambalo linalotukwamisha na kutuvunja moyo vijana wengi katika kufikia mafanikio yetu. Historia za nyuma zinazo husu kushindwa kwetu katika biashara, mashindano au kitu chochote ambacho tulikifanya kama njia yetu ya kutoboa tobo la mafanikio zinatufanya tunakuwa watu wakukata tamaa na kurudi nyuma hivyo kama unataka kutoboa katika maisha yako ni lazima ufute hizo historia kuweka mwanzo mpya na kuongeza nguvu ya kufika katika mafanikio yako.
- Anza kufanya kwa kujiamini na kwa uhakika fanya bila kuchoka, ni muhimu kujiamini na kuamini kile unachokifanya kwani wewe ndiye unaejua uendako na umuhimu wa unachokifanya hivyo kile unachokifanya kiamini na ukifanye mpaka mwisho, jambo litakalo kusaidia kufikia malengo na kuwafanya wasio kuamini waamini na kujifunza kutoka kwako.
- Jua wazi kuwa wewe ni mfano kwa wengine, amini amini nakwambia kuamini katika kile unachokifanya ni moja ya silaha kubwa katika kuelekea mafanikio yako usikazane kusoma nani alifanya nini akafanikiwa kwani kila mmoja anakipawa chake katika utendaji wa kazi zake hivyo kujiamini na kukamilisha majukumu yako ipasavyo itakufanya siku moja mtu mwingine ajifunze kutoka kwako. Amini wewe umezaliwa kuwafanya watu wajifunze kutoka kwako.
Mbali na hayo yote ambayo
tunaamini ni njia za kutufanya kufikia malengo ni muhimu sana kwa kila kijana
popote unapokuwa kufahamu wazi kwamba biashara au kipaji ulichonacho hakiwezi
kukua kwa kukazana kusoma maneno yakukutia moyo kutoka kwa waliofanikiwa au
waamasishaji bali mafanikio yako yakweli yapo katika uthubutu wako na maamuzi
pamoja na utendaji kazi wako wa dhati katika kila jambo ambalo unaamini ndio
njia ya mafanikio hivyo soma kidogo fanya kazi kwa wingi heshimu kila mtu anaefanya
ufanikishe kazi zako.
Vijana mbona mambo yente
Kwa mada tamu kama hizi usisite
kutufollow kwenye blog yetu
Ze
potential info.
Nelsoncharlesmatagi.blogspot.com
2 comments:
Ujumbe umeeleweka
kwa hakika
Post a Comment