Breaking News
recent

LINZA WA MAMA

Simulizi sehemu ya Tatu
 ilipo ishia 
Juma anakubali kuzaa na Linza huku Linza akiwa anamashaka juu ya familia yake  
sasa endelea..
  • Msimulizi : Juma A.K. A J kama ambavyo Linza anavyomuita amekubali kuzaa na Linza ila Linzaanakumnbuka hali ya nyumbani na maono ya wazazi wake, hali hiyo ilimfanya akumbuke vizuri ushari wa Avijawa na Zubeda akautoe ujauzito huo. Linza anaamua kwenda kwa siri kwa mashoga zake kwenda kutimiza hazma yake ya kuutoa ujauzito huo,kutokana na hali ngumu ya maisha wasichana hao wanaamua kutumia dawa ambazo sio sahihi kwa kazi hiyo na kusababisha maumivu makali ya tumbo na damu kuanza kmtoka nyingi sehemu za siri za binti Linza

LINZA : (ANALIA KWA uchungu huku akiomba asaidiwe)
ZUBEDA : kwani ulimpa vidonge vingapi?
Avijawa :  kama ulivyosema kumi tu.
Linza : (anaongeza sauti ya kuugulia na kulia kwa maumivu)
 Zubeda : Linza nyamaza ngoja tukupeleke hospitali
Avijawa : Zubeda ni kesi hii ooh!!!
Linza : (anaongeza sauti ya juu na kulia zaidi)
Zubeda : Avijawa mshike huko tumpandishe kwenye  bajaji chapu (aliongea mfululizo huku ana hema kwa hofu)
  • Msimulizi : ooh!!  Maskini Linza ...!! ni siku ya tatu sasa tang Linza apelekwe hospitalini hapo. Anapata fahamu na kukutana na sura ya baba na mama yake na kwa pembeni akiwa amesimama Juma . baada ya kuamka Juma alichomoka mbio na baada ya dakika aliludi akiwa ameongozana na daktari.

Daktari :  ameamka si ndio..?
Juma : ndio daktari
(akafika, daktari akampima mgonjwa na kuendelea)

Daktari : hali yake kwa sasa iko vizuri niwatoe hofu kuwa mgonjwa wenu yuko salama.(anamgeukia mgonjwa) vipi  Linza unajisikiaje na wapi panauma.
Linza : najiskia vizuri ila mgongo na hapa chini ya tumbo panauma kiasi
Dactari : usijari hayo maumivu ni kwasababu umelala mda mrefu na kunaupasuaji tumeufanya hivyo utakuwa sawa usijari
Linza : asante
Daktari : okey basi mnaweza kumuandaa mgonjwa na mje ofisini kwaajiri ya kupata ripoti kamili.
  • Tukiwa tunaenda ukingoni mwa hadithi hii tunakukaribisha yeyote mwenye hadithi yake atume tuipe nafasi kwenye blog yetu.

No comments:

Powered by Blogger.