Breaking News
recent

Kwa jinsi gani kijana wa chuo anaweza kujitunzia akiba kwa matumizi ya baadae..

Image result for equilibrium

                                                                                                         Na  Emiliana Michael
  
  • Kila mwaka  vijana zaidi ya elfu 20 hujiunga na elimu ya juu (vyuo vikuu) nchini Tanzania ambao wanakua wamekidhi vigezo vya kujiunga na elimu ya vyuo vikuu. Lakini vijana Hawa wengi hawajui umuhimu wa kujiwekea akiba japokua ni wasomi.
  • Kujiwekea akiba ni suala ambalo kila mtu anatakiwa kufanya,sio wanafunzi tu,bali kila mtu anatakiwa kujiwekea akiba kwani ni mtaji wa baadae.Zipo njia nyingi ambazo mtu anaweza kutumia ili kujiwekua akiba,moja wapo ikiwa ni kuweka pesa benki,kutunza kwenye vibubu,na wengine huweka kwenye mitandao ya simu za mikononi.
  • Kwa upande wa wanafunzi wa vyuoni, wanaweza kujiwekea akiba kwa kufanya kitu ambacho kitaweza kuzalisha pesa na kupata faida na hatimae kutunzaa faida iliyopatikana, kuwa na mpangilio wa matumizi ya pesa zao ili kuepuka matumizi mabaya ya pesa, pia kuwa na nidhamu ya pesa ni Jambo la msingi sana katika maisha ya kila binadamu ili kufanikiwa nidhamu ya pesa inatakiwa sana.
Image result for tanzania shillings
Kumbuka waswahili husema akiba haiozi,maana yake ni kwamba ukitunza  Sasa utatumia na baadae.Hata matajiri wa kubwa duniani walianza kwa kuweka akiba na kuwa na nidhamu ya pesa.
(Picha mtandaoni)

No comments:

Powered by Blogger.