BAADA YA HAPA MIMI NA WEWE BASI
Na: EMILIANA EDMUND
Hujambo mpendwa msomaji wangu,leo nimepanda kitu kizuri kwa
ajili yako na mwenza wako kitakacho kufanya upate mustakabali wa hayo maisha
mnayoishi kwa kipindi hiki,ili kuwapa picha halisi ya maisha yenu ya hapo
baadae mtakapokua katika ndoa.
Leo nataka tuegemee upande wa wewe ulie na mahusiano ya
kimapenzi na mwenza wako alieko chuoni,yaweza kuwa wote mko chuo au mmoja kati
yenu yuko chuo.
Wakati mtu anapofika chuoni tunaimani kwamba kitu kikubwa kinachokufanya
wewe uwe pale ni kwasababu ya kusoma lakini linapokuja swala la kuwa na mpenzi
hizo zinakuwa ni tamaa ambazo kama ukitaka zinaweza kuepukika.
Vijana wengi wamejikuta wakiingia katika majuto na kwa
upande wa wasichana wamejikuta wakipata mimba zisizotarajiwa kutoka kwa hao
wapenzi ambao wamekutana vyuoni. Kumbuka kwamba huyo mwanaume au mwanamke umekutana
nae hapo chuoni,huyajui maisha yake vizuri wala kwao hupajui, unakuwa nae kwa
muda wote hapo chuoni mnaishi kama mume na mke,baada ya kuwa mmemaliza kipindi chenu
cha masomo kila mtu anarudi kwao na wengine kutojuana kabisa.
Kumbuka kwamba chuoni ni mahali ambapo hadi wenye familia
zao wapo hapo sasa unajikuta uko katika mahusiano na mume wa mtu anakupa mimba
huku akikudanganya kuwa atakuoa na wengine kukutambulisha kwa marafiki zake ili
kukulaghai kwamba anakupenda kwa dhati.
Mchunguze sana huyo mwenza wako je,ni kweli anakuitaji kimapenzi
au kimaisha?, Je ni mtu anayependa kukuweka wazi katika mambo yake au ni mtu msiri
sana,anakuruhusu kushika simu yake?.
Hivi ni baadhi ya vitu ambavyo unaweza
ukachunguza na kujua kuwa ni ukweli anakupenda kwa dhati au anataka kukuchezea
na kukiacha.
No comments:
Post a Comment