Natamani tuishi wawili
Na
Charles N Matagi
Tunafanya
kama utani, ukweli unapenya ndani
Hicho
chako kisirani, nakipoza na matani
Njoo
wangu uwe wa ndani, tuyazungumze kitandani
Nakupenda
si utani, punguza tafarani
Nikuite
jina gani, maana yote yapo ghalani
Mpenzi
au mwandani, yote yapo moyoni
Penzi
langu la sirini, leo naliweka hadharani
Nakupenda
si utani, tafadhali niweke moyoni
Uzuri
wako wa asili, tabasamu lako sawili
Nakupenda
nakiri, kwa wengine nimeghaili
Natamani
tuishi wawili, tusiwasikilize waswahili
Watatuletea
timbwili, moyo wako wataukatili
Jicho,
pua, midomo, nyusi, nyuma umejaza kiasi
Una
utamu wa nanasi, nimesahau mafenesi
Naitaji
Zaidi nafasi, nikutoe wasiwasi
Achana
na hao wazushi, nakupenda kupita kiasi
No comments:
Post a Comment