Breaking News
recent

WALA SIKUTAMANI WEWE..(Shairi)


Image result for broken heart
Na Charles N Matagi
Raha mapenzi safari, mala tendo nalifurahia
Huku hali yangu si swari, sikufichi nakuchukia
Mimi sio jabari, moyo wangu nkakuachia
Acha niwe kiburi, shimoni ntakufukia

Ulianza polepole, kwa kasi ukaniingia
Nia yako unipole, amani nliyo shikilia
ulipiga vigelegele, nanga kwako nlipotua
leo napiga kelele, ukinifata ntakufyatua

kwa penzi lako barafu, lilinifanya kipofu
hakika nilidhoofu, nikakupenda maradufu
ukani visha sikafu, hiliyo jaa sihafu
ulinichezea rafu, michezo yako michafu

kwangu ulifata nini, hili nataka kujua
mbona nilikuthamini, nini kilicho pungua
ukanishusha thamani, donda ndugu ukaniachia
wala sikutamani, haki ya nani naapia

sasa naruka mwenyewe, mbawa zangu natumia
wala sikuitaji wewe, roho yangu imetulia
bora niishi na jiwe, mgongoni ntakunia
acha niwe mwenyewe, hali yangu ntapambania.

No comments:

Powered by Blogger.