TAMU KOMAMANGA MOYONI LIMEPOTE (Shairi)
Na Charles N Matagi
Maisha magumu ndio
chanzo, penzi kudidimia
Nilipofeli mipango,
ukutaka kuvumilia
Ulimfata mzee jongo,
mbali ulinitupilia
Sasa nimepata michongo, penzi limeteketea
Shida ukustaili, pekee
ulijiwaza
Ni kweli auna akili,
ulishindwa kujitunza
Moyoni nlistaimili,
ukuchoka kunikwaza
Ulitoa wako mwili,
hakika ulijiuza
rafiki yangu Fikiri,
utamu ulimpatia
Juma na jabiri, mwili
wako wanaujua
Niliyafanya siri,
moyoni nikagugumia
Yote hayo nakirii,
ukweli nliujua
Zuri langu komamanga,
mchangani limeangukia
Limejawa mchanga, watu
wanalikimbia
Mimi sasa nimuhanga,
maumivu naugulia
Lile tamu komamanga,
moyoni limepotea
No comments:
Post a Comment