Kwa
picha ya haraka mtu anaposikia neno "Rastaman" anamuona mtu mweusi
mwenye msokoto au msuko wa nywele ndefu, ngumu na za asilia, anaona bangi na
muziki wa Reggae. Watu wengi wanafikiria kwamba Rastaman ni muhuni fikra ambayo
si kweli, Rastaman si muhuni kama wengi wanavyodhani.
- Kwanza
kabisa Rastaman(mtu rasta) ni mcha Mungu kwani huziheshimu na kuzifata amri za
Mungu, Rastaman(mtu rasta) anafanya ibada kama watu wengine wanavyofanya ibada
zao, japo watu wengi hudhani kwamba Rastaman(mtu rasta) hafanyi maombi.
Rastaman anapata mkate wake wa kila siku kwa kufanya kazi, kazi za arts mfano
muziki, kuchora, kuchonga, kufuma na kazi nyingine nyingi.
|
HAILE SELASSIE I |
- Rastaman
ni mtu mpenda umoja na amani, ninaposema hivyo nina sababu inayonifanya niseme
hivyo kwani mwaka 1980 katika wa siku ya uhuru wa Zimbabwe, Bob Marley alipata
nafasi ya kuimba wimbo wake "Africa Unite" wimbo unaohamasisha umoja
wa Africa, "how good & pleasant it could be before God & Man to
see the unification of Africa" ni kimstari kidogo kwenye wimbo huo
kinachotaka umoja wa Africa.Viongozi wa Africa waliupenda saana wimbo huo.
- Rastaman
ni mtu asiependa uonevu, ni mtetezi wa wanyonge, ni vigumu sana kwa rastaman
kuona mtu anaonewa mbele yake kwa mfano Jah Rastafari(Haile Selassie I kama
anavyojulikana kwa jina la ubatizo) 1935 Italy chini kiongozi dikteta Mussolin
Benitto alipo ivamia Ethiopia kwa mara ya pili Haile Selassie I alikimbilia
Uingereza ilikujipanga kurudi kuikomboa Ethopia chini ya Italy, 1936 alipata
nafasi ya kutoa hotuba mbele ya umoja wa mataifa alisema “mbali na ufalme wa
Bwana hakuna Taifa ambalo liko juu ya taifa jingine, leo ni sisi, kesho ni
wewe.”kauli ambayo ili hamasisha kupinga unyonyaji na fikra kandamiz ambapo
mwaka 1945 Haile Selassie I alifanikiwa kuikomboa Ethopia kutoka mikononi mwa
dikteta Mussoline. Salamu za ki rastaman zenyewe zinahamasisha amani mfano " Amani - peace & love forever" au Haile Selassie I - Jah
Rastafarian". sasa inakuaje
Rastaman anaonekana muhuni!!
- Uhusiano
wa bangi na Rastaman ,hii ndio sababu inayofanya watu waone kwamba Rastaman ni
mtu muhuni. Kwa imani ya ki rasta bangi ni sankramenti na sankramenti ni kitu
kinacho heshimika na kutumika kwa kila imani, rastaman anapovuta bangi anapata
morali ya kufanya kazi kwa bidii na ifahamike kuwa hakuna Rastaman anaevuta
bangi na kwenda kufanya fujo au kuvuruga
aman popote pale kwani bangi kwao hutumika kukamilisha ibada na
tahajudi(meditation) na ndio maana Luck dube katika wimbo wake wa “Rastaman’s
prayer” aliimba “those that smoke marijuana(bangi) wanna thank you Father for
making it grow internationally… even though police cut it down but it grows
again thank you Father”. Alimshukuru Mungu kwa kuifanya bangi ikalimwa
kimataifa japo kuwa inapata changamoto mfano police wanaikata na kuichoma
lakini bado inaota tena, Hivyo bangi kwa Rastaman ni sakramenti na ijulikane
kwamba sio kila Rastaman anavuta bangi.
|
BOB MARLEY |
|
Marijuana(jani la bangi) |
- Hivyo wazo la kuwa Rastaman ni mtu muhuni tuu sio wazo sahihi. Rastaman ni mtu mkarimu ,mpole na mcheshi , ni mara chache sana kuona Rastaman anagombana au anazozana.
- Mbali na
hayo Rastamans wanaonekana kuwa wakorofi
na wahuhuni kwa kuwa ibada zao wanafanya kwenye maeneo ya wazi na hawataki
kuingiliwa wanapokua ibadani, ni wazi kuwa hakuna mtu anae taka kuingiliwa
anapokua anazungumza na Mungu wake.
No comments:
Post a Comment