Leo ni siku yako kijana.
Na Charles N
Matagi
Naangalia kesho,
kesho yako kijana
Nayaona mateso,
kama autopambana
Utashindwa inua
uso, kwawale wanaokutazama
Leo ni siku
yako, unapaswa kupambana
Miaka mingi
shuleni, mpaka chuoni umezama
Mbona aupo
kileleni, jahazi lako linazama
Tunasahau
dhumuni, la wewe kwenda kusoma
Leo ni siku
yako, unapaswa kukomaa
Shule ufati
ajira, acha zako lawama
Unapewa tu dira,
ya kuweza kusimama
Basi fanya
himahima, kabla ya jua kuzama
Leo ni siku
yako, timiza ndoto zako
Zama
zimebadilika, kaka shtuka
Usitandike mkeka,
anza kufanya hekaheka
Utatoboa haklika,
siku yako imefika
Leo ni siku
yako, okoa kizazi chako
Futa machozi
yako, kaza mkwiji wako
Ongea na nia
yako, tumia na nguvu zako
Ukane udhaifu
wako, dhiilisha uhodari wako
Leo ni siku
yako, kamilisha ndoto zako
Tumia elimu
yako, kusaidia wazazi wako
waliwekeza kwako,
uwaondolee sikitiko
Tumia ujuzi
wako, kusaidia jamii yako
Kwani leo ni
siku yako, pigania muda wako.
No comments:
Post a Comment